Hello ndugu yangu msaka hekima ndani ya Madini Media, natamani sana nikusalimu kwa lugha yako ya kikabila…!!, baada ya bidii kuangukia ziro basi turudi zetu kitaifa kupiga
stori mbili tatu na kijana adim sana, mkazi wa
Arusha na anafanya muziki wa Hip-Hop, jina lake
ni Okaluti Candle!
Wataalamu wa muziki wanamtaja Okaluti
kama msanii mwenye nidhamu ya kiwango cha juu
katika sanaa, kwa jinsi anavoheshimu na kuenenda
katika misingi ya kile anachofanya na kujilinda asijikwae
katika neno lolote, mwepesi wa kuchunguza maandiko
na kujirudi pasipo kusubiri.
Amini kuwa leo ameketi pamoja nami katika meza ya duara ya Madini Media, ili
apate kutujuza mengi aliyonayo moyoni kama anavyodai, hivyo sitamfanyia mahojiano zaidi ya kumpa
nafasi yeye kufunguka kadri anavoweza,
nakualika sasa kuketi pamoja nami ili tuskie
toka kwake.
KARIBU OKALUTI,
Ookay asante sana, mi naitwa Okaluti Candle, nafanya muziki chini
ya Like My
Light! Leo nimetamani kujibu swali la
wengi kuhusu mziki wangu, kuwa siendani na game au nashindwa
kubadilika kuendana na wakati. Niombe radhi kwa mashabiki wangu, sababu
nimekuwa mkaidi kwa ushauri wao na nyongeza ya hapo ni kwamba siwezi
badilika kuendana na upepo sijui. Nipo nitadumu kwa misingi na hizi ni nguzo
imara juu ya mwamba, sibabaishwi na upepo. Wengine wanadai eti nitabaki maskini, wamesahau kuwa
niko
tayari hata ikigharimu maisha yangu. Mashabiki na wafuasi wa muziki
wangu, sipendi msijue ya kwamba Muziki ni Kirusi au Roho Kamili, usipokuwa makini unakutumikisha.
Mwanadamu anaposhiriki damu ya vampaya ama kwa kungatwa au
kuchanjwa, basi hubadilika na kuwa na tabia za vampaya. Katika mabadiliko haya
anaweza asijitambue kabisa na anaweza kufanya tukio kubwa la kusikitisha
asitambue ni yeye hata anapoambiwa baada ya uvampaya kutulia anaweza kuwa
mbishi sana. Hali ya mtu huyu huendelea kuwa mbaya kila siku kwa kadri virusi vilivyomvamia
vinavoendelea kukua na kuzaliana ndani ya mwili wake. Kwa sababu tayari
ni mwathirika, katika hali ya uvampaya hujikuta anawaambukizia wengine hata
ndugu zake na watu wa karibu yake na mwishowe unakuta jamii nzima inayomzunguka
wameathirika na kuwa mavampaya.
Kama ilivyo kwa vapaya, vivyo hivyo na muziki
ni kirusi au roho kamili inayoweza kumuingia mtu kupitia
masikioni au machoni na kumbadilisha hata kumtumikisha.
Jiulize unapokuwa Club alafu ikacheza trak ya Juma Nature, hapo kumpata kijana
wa kiume ameketi ni nadra sana, au iwekwe Ndi Ndi Ndi ya Jide hakika hakuna wa
kike atakaesalia kwenye kiti. Hatari ni pale inapochezwa Muziki ya Darassa
mahari popote pale, hakuna cha Pombe wa Magu wala Baba wa Upako,
wote hawa wanajirusha pasipo kujali cha cheo, nafasi walizonazo wanazisahau na
kuutumikia muziki, na ukiuzima mziki ndipo wanaanza kujishangaa walichokuwa
wakifanya.
Hizo ni track za kuparty zinawapelekea watu kupaty
pasipo kujizuia wala kujielewa sababu sio wao tena wenye maamuzi
bali ni
ile roho au kirusi kilichowavamia. Na
vipi kuhusu track ya uchochezi, hapo lazima ushuhudie raia wakibeba silaha
za kila aina na wakati mwingine wanaandamana kuvamia ofisi husika.
Hii ndio sababu kuu ya BASATA kufungia baadhi ya kazi za wasanii zinazoonekana
kukiuka maadili husika, maana ukiziruhusu utakuta jamii nzima wanafanya mambo
ya ajabu kutokana na kazi moja tu inayokiuka maadili uliyoiruhusu kusambaa. Hii
yote ni kwa sababu muziki ni roho kamili
inayoweza kumuatack yeyote kwa haraka sana na kuleta madhara makubwa,
si kwake tu bali kwa jamii nzima katika wingi wake.
Niseme nini basi juu ya track zinazohusu wanawake na maendeleo
na hata sasa tunayaona matunda yake, pongezi kwako malkia wa nguvu. Kushoto
kwangu kuna mmoja ananikumbusha ile ya mtoto wa kiume niache nijitume, na
wengi waliobahatika kufikiwa na hii track walihamasika kutafuta. Kipindi cha
nyuma zimesikika track kama jukumu letu na amka mtanzania ambazo zimewazindua
wengi usingizini walipokuwa wakiota kuwa maendeleo yanaletwa na
viongozi. Miziki imekuwa ni faraja katika misiba na katika hali ya
huzuni, miziki imetumika mara nyingi sana kuimarisha na kuboresha mahusiano ya
wanandoa. Kwa habari ya injili, imevuta wengi katika mikutano na makanisani. Miziki
imekuwa ni chachu ya furaha katika sherehe na harusi.
Niseme nini basi juu ya hii miziki ya ‘inama kidogo, shika magoti’ kwa
kuwa
ni kirusi lazima dada zetu watainama tu na
kushika magoti, na dakika si nyingi tunaskia wakiwasifia et ‘unanitekenya
ukinyonga’. Niwakumbushe tena jamani Muziki ni
Roho kamili, unakutumikisha bila udhuru. Sasa na
hizi story za chumbani zinatufikiaje huku, au ndo umbea wenyewe, mke na mume
wote wanauchonga. Utaskia et eiii, akaja chumbani na kangamoja akaidondosha, basi kitandani sodoma
na gomora. Aya huyu nae anambwambia nanii wake chumbani hata nje
tunaskia, et ooh ‘gusa nimeshapagawa tena na tena nitawale kiuno’. Hii miziki
inaskilizwa na kutazamwa na watoto na vijana wa kiume na wakike, na roho hii inapowaingia huwa inawatumikisha sawa sawa.
Hakuna utumwa mbaya kama
kutumikishwa kwa ngono. Utumwa wote hufanyika kwa mwili nje ya
mwili, ila ngono ni utumwa unaopenya ndani ya mwili kuidharirisha soft ya uzazi,
kisha hupenya katika akili na kumuharibu mtu kisaikolojia. Mabinti
hawa utakuta wanabadilika na kuwa na majivuno, huanza kujikweza, dharau
nyumbani hata kwa wazazi wao maana hakuna asichokijua km kukatika amejua na tiyari
kasifiwa. Kwa wanafunzi, awe wa shule ya msingi, sekondari au chuo, mara
nyingi roho hizi zinawafanya washuke kitaaluma na
kushindwa kufanya vizuri katika mitihani yao, na hii inawafanya kuendelea kuwa
watumwa wa ngono ili wajaziwe vizuri. Kumbuka hii yote chanzo ni miziki.
Hizi roho zitokanazo na miziki ya
mapenzi zinapokuingia na kukufanya mtumwa wa zinaa, hapa
ndipo pia mshahara wako utakuwa ni mauti na kabla ya kufa ni laana
na magonjwa. Hizi takataka kama Kansa na Ukimwi kwani zinaenea kwa njia
gani? Vipi kuhusu kubeba na kutoa mimba? Vipi kuhusu
madonda ya tumbo sababu ya msongo wa mawazo kisa mpenzi wako sio
mwaminifu? Hivi sio wewe ulietusimulia habari za waliouana kisa wivu wa
mapenzi? Je kwa hali kama hii kuna usalama gani kwa watoto wetu? Vuta
picha, vijana wetu wana hali gani? Maana hawaishiwi kufundishwa tu
kupitia muziki, wanahamasishwa na wakifanya kwa bidii wanasifiwa.
I’m so sorry, I can
imagine how yo fell! Tuliza sasa mawazo nikupe tiba ya hawa virusi na jinsi
ya kuthibiti hizi roho kamili. Tatizo
sio muziki hata kidogo, tatizo lipo katika aina
ya muziki unaosikilizwa au kutazamwa na mlengwa. Kama ni wasanii basi
tuzalishe kazi zenye kuleta matokeo chanya katika jamii, kama
walimu tuifundishe jamii kuenenda kimaadili. Tusiweke mbele maslahi,
maana laki tano ya
show haiwezi kununua roho za vizazi unavyoangamiza kila siku.
Kwa upande wa pili, tuache ushabiki wa kipumbavu, kushabikia miziki ya bhangi,
madawa, zinaa na matusi. Hata redioni tuombe track za kisiasa, kimaisha, injili
na za
kuelimisha au kuhamasisha matokeo chanya.
Maandiko yanasena, ‘kinywa cha mtu hutoa yaujazaoyo moyo wake’
na haya
ndio yaliyonijenga kwa imani hai, maana isiyo na matendo imekufa. Hii ndio
sababu nimeshindwa kuendana na upepo wa game maana mi nimejengwa juu ya
mwamba kwa misingi na nguzo imara. Siwezi kuimba maneno ya aibu
na kuwavalisha
dada zetu vichupi eti kisa nipate air-time na hivyo vilakilaki vya show.
Kufanya hivo ni kuua kizazi hadi kizazi maana muziki haufi, bunduki inaua mmoja
mmoja ila muziki unaua vizazi HADI vizazi kwa jinsi unavoishi, kukua
na kuenea. Ukiweza Download track zangu, zote nimeimba kuhusu maisha na kimaadili
zimehaririwa na Like My Light! Zote ziko
(HAPA)
OKALUTI CANDLE - ALL TRACKS
Binafsi nimepata kitu kipya,
vipi wewe ndugu, maana ni muda mrefu nimekaa pembeni na kumwachia nafasi Okaluti ili kwa pamoja tuthibitishe maneno ya wachambuzi wa sanaa
juu ya kile wanachoamini kuwa Okaluti ni mwanamziki mwenye nidhamu sana zaidi ana uwezo mkubwa wa kufikiri.
Nisijue kwako imekuwaje, ila mimi
nilikuwa darasani, na sasa nikushukuru wewe ulieketi nami kwenye meza ya Madini Media katika kusikiliza hekima ya Okaluti Candle, zaidi nakusihi usiondoke bila kutembelea vipengele kadhaa katika blog hii,
na jitahidikufanya hivo kila siku, Thanks for your
company.
©M(L)30MA17-02
Source: Okaluti Candle
Edithor: Samson P. Duttu
Allowed: Share, copy&paste
Don’t try: To edit any.



0 Maoni