NA.MWANDISHI WETU
Taifa la Botswana limelifunga kanisa la
muhibiri mmoja wa Malawi mwenye utata anayedaiwa ''kutembea angani''.
Serikali ilithibitisha kufungwa kwa kanisa la
Bushiri la Christian Gathering Church ECG mjini Gaborone mara kadhaa kutokana
na wasiwasi kuhusu ''fedha za miujiza''.
Chombo cha habari cha Malawi24 kimeripoti
kwamba kanisa hilo lilipinga uamuzi huo mahakamani uliochukuliwa chini ya mwaka
mmoja baada ya muhibiri huyo kupigwa marufuku kuingia nchini humo.
Alikuwa ametarajiwa kuhudhuria kongamano
fulani.
Hatahivyo waziri wa Botswana Edwin Batshu
alitangaza mnamo mwezi Aprili 2017 kwamba bwana Bashir ambaye sasa anaishi
Afrika Kusini atahitaji Visa ili kuingia, licha ya raia wa Malawi kutohitaji
kibali hicho kulingana na chombo cha habari cha AllAfrica.com
Serikali imetangaza kwamba kanisa hilo
litafungwa kabisa, huku gazeti hilo la Botwana likipata barua ilioambia
usimamizi wake kwamba kibali cha kuendesha kanisa hilo kimefutiliwa mbali.
Gazeti hilo limeongezea kwamba ni hatua ya
kanisa hilo kutumia ''fedha za miujiza'' ambayo imevunja sheria za taifa hilo.
Bwana Bushiri ambaye ana zaidi ya ''likes''
milioni 2.3 katika mtandao wa facebook na ambaye alivutia umati mkubwa wa
kuweza kujaza uwanja wa FNB mkesha wa mwaka mpya bado hajatoa tamko lolote.
Kanisa hilo ni maarufu kwa mtindo wake wa
maisha ya kifahari kutokana na ufanisi wake ambao umevutia wafuasi wengi barani
Afrika.
Alishutumiwa mwaka uliopita baada ya kubainika
alikuwa akiwatoza kati ya dola 80 hadi 2000 wafuasi wake waliotaka kuhudhuria
chakula cha jioni naye kulingana na chombo cha habari cha Afrika Kusini South
Africa News24
SOURCE.BBCSWAHILI.COM


0 Maoni