NA.GOODLUCK CHRISTOPHER
Nimatumaini yangu umzima waafya na kama kawaida
tunakutana tena katika makala nyingine tena lengo ikiwa ni kupeana elimu kwa
kile usicho kijua na kama unakijua basi tunakuongezea maarifa napenda
kukukaribisha wewe pamoja na jirani yako kwani mambo mazuri yanapatikana huku
karibu sana.
Kigoma ni moja kati ya mikoa zaidi ya 30 katika nchi
ya Tanzania, Mkoa huu unapatikana magharibi mwa nchi ya Tanzania huku ukiwa
umezungukwa na mikoa ya Tabora,Katavi,Kahama pamoja na Kagera.
Mkoa huu una patikana pia mpakani mwa nchi kama
Rwanda,Burundi pamoja na Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo hivyo huwa ni rahisi
kwa watanzania kusafiri kwenda nchi hizo ama watu kutoka nchi hizo kuingia
Tanzania.
Kwa asili mkoa huu una makabira ambayo ni Waha,Wamanyema,Watongwe, wabwali, Wajiji
n.k huku yakifatiwa na makabira machache mengine kutoka mikoa mingine ya
Tanzania Lakini pia wakimbizi kutoka nchi ya Kongo,Burundi pamoja na Rwanda.
Mkoa wa Kigoma una wilaya zisizo pungua………… ambazo
ni Halimashauri ya manispaa ya kigoma ujiji, Kasulu, Buhigwe, Kibondo pamoja na
Uvinza na zote hizi zikiwa zina ukamilisha mkoa wa kigoma.
Mkoa huu umejaliwa vivutio vingi vya utali ambavyo
ni Milima unayo uzunguka mji wa kigoma,Ziwa,Mbuga za wanyama, Chuvi, Mto
maragalasi,Vyura wanao nyonyesha nah ii ikiwa ni maajabu makubwa sana na vingine
vingi vinavyo patikana.
Shughuli zinazo fanywa na wakazi wa mkoa huu ni
Kilimo,Uvuvi,Ufugaji na kazi za viwandani pamoja na maofini lengo ikiwa ni
kujipatia kipato kama ilivyo kwa mikoa mingine.
Ziwa Tanganyika ni ziwa pekee linalo patikana mkoani
kigoma na likiwa ni ziuwa pekee lenye kina kirefu duniani, Mbali na ziwa hili
kupatikana sehemu kubwa ya kigoma limepakana pia na mikoa kama Ktavi na sehemu
ndogo sana ya mkoa wa Mbeya huku ukipakana na nchi jirani kama Kongo,Burundi na
Zambia.
Ziwa Tanganyika linasifiwa kwa kuzalisha samaki
wengi na wazuri kama migebuka,Dagaa wa kigoma n.k ambao wanatoa furusa ya ajira
kwa vijana wengi wa mkoa huu pamoja na kupata kitoweo kizuri kwa wakazi wa mkoa
huu na nchi kwa ujumla.
Mv.Lyemba ni moja kati ya meli kongo ambayo imekuwa
ikifanya safari zake ndani ya ziwa Tanganyika kwa kuwasafirisha watu pamoja na
mizigo kati ya mkoa wa kigoma kwenda nchi jirani kama Burundi, Kongo na Zambia
toka enzi za mkoroni.
Kama ilivyo kilimo ni uti wa mgongo basi wakazi wa
mkoa huu kilimo ni sehemu ya maisha yao ambapo watu hujishughulisha na kilimo
kwa asilimia kubwa hususa ni maeneo ya vijijini kwasababu mkoa huu una aridhi
ya kusiwisha mazao mbalimbali kama Mahindi,Maharage,Kahawa,Tangawizi,Michikichi
na mazao mengine mengi.
Vivutio vya utali basi kigoma ndo mahali pake kama
nilivyo kutajia pale juu na kubwa zaidi ikiwa nimbuga za wanyama kama Gombe
mbuga inayopatikana juub ya milima inayo lizunguka ziwa Tanganyika na ikiwa
imesheheni wanyama aina ya Sokwe mtu.
Lakini pia Mahale nayo pia ni hifadhi ya wanyama
pori ambayo pia imelizinguka ziwa Tanganyika ambapo watalii wengi hupenda
kufika huko kwa kutumia usafiri wa Boti huku wakijionea manzali nzuri ya ziwa
lenye kina kirefu duniani pamoja na samaki wa aina tofauti tofauti.
Hivyo ni baadhi ya vivutio vinavyo patikana mkoa huu
wa kigoma ambavyo watalii kutoka nje na ndani huja kujionea huku seerikali
ikiingiza mapato kwaajili ya utali wandani na nje.
Mji wa Ujiji ni moja ya mji mkongwe ambapo ni sehemu
ya kihistoria ambapo Dkt.Living Stone alipata kuishi katika eneo hili lakini
pia sehemu aliyo pata kuishi mpaka leo hii pamehifadhiwa na watu mbalimbali
hufika hapa na kujionea baadhi ya vitu ambavyo Living Stone aliacha.
Ukarimu ni sehemu pekee ya wakazi wa mkoa huu hakika
ukifika katiika mkoa huu utapata kujionea ni jinsi gani ni wakarimu na wanavyo
ishi kwa kujariana kwa mambo yanayo ihusu jamii ya kigoma.
Uchapa kazi ndiyo sifa kuu ya wakazi wa mkoa huu
ikiwa ni wakiume,wakike na hata wato ni watu wanaopenda kujishughulisha katika
majukumu mbalimbali lengo ikiwa ni kujipatia kipato cha kujiendeshea maisha
yao.
Asili ni moja ya kitu kinacho zingatiwa na hususa ni
lugha hakika ukifika hapa utaweza kuzungumza lugha ya kiha tena kwa siku chache
kama ilivyo kuwa kwangu tena ni rugha nyepesi sana ambayo ukijua utaweza
kuongea na watu wa aina tofautitofauti wa kibantu mfano.
Wakongomani,Wanyarwanda,Wahangaza,Warundi pamoja na Wahaya lakini pia Waganda.
Uasili wa vyakula bado uppo mpaka mjini huku unapata
ugali wa mhogo pamoja na mafuta ya asili aina ya mawese ambayo hayajachanganywa
na kemikali zozote ambayo pia inasemekana ni Dawa ya macho kwa wale wenye uoni
hafifu mimi nimesha tumia nimeamini nikweli mafuta haya ni dawa.
Mawese ni mafuta ya kupikia ambayo yanatokana na
mumea aina ya mchikichi ambapo hukamuliwa matunda yake yakiwa yamekomaa na
kuzalisha mafuta hayo.
Wakazi wa mkoa huu wanapenda sana kula Samaki kuliko
Nyama kwasababu samaki wanapatikana kwa wingi na huku wengine wakiamini kuwa
samaki wazuri katika kujenga mwili kuliko Nyama.
Uwanja wa ndege ni moja wapo ya sehemu ambayo watu
wengi huitumia kwenda sehemu mbalimbali kwa haraka kwamfano mikoa mingingine
kama Dar es salaam ,Mwanza,Mpanda,Arusha n.k lakini pia nchi za nje kama DUBAI
ambapo wafanya biashara hutumia uwanja huu kupokea mizigo yao.
Mkoa wa kigoma kwa sasa barabara nyingi za mjini
pamoja na zinazo unganisha wilaya lakini pia mikoa baadhi yake tayari
zimekwisha jengwa kwa kiwango cha lami jambo linalo warahisishia wakazi kutoka
sehem moja kwenda nyingine.
Gari moshi ni mkombozi kwa wakazi wa kigoma pamoja
na nchi jirani kama Burundi na Kongo ambapo watu hawa husafiri na kusafirisha
mizigo kupitia reli ya kati kwa urahisi na gharama nafuu.
Wilaya ya Uvinza imejizolea umaarufu kwa kuwa na
viwanda vingi vya kuzalishia chumvi ambapo pia viwanda hivyo vimebeba ajira za
vijana wengi kutoka ndani na nje ya mkoa wa kigoma.
Lakini pia wilaya hiyohiyo inasifika kwa kuzalisha samaki wazuri kutoka
mto Malagalasi lakini pia kuzalisha ugari wa lowe utokanao na zao la mihogo
vitu ambavyo hupendwa zaidi na wakazi wa mkoa huu pamoja na wageni.
Wilaya ya kasulu imejizolea umaarufu kwa kuwa na
wawekezaji wengi hususa ni wafanya biashara ambao wameifanya kuwa mji wa
kibiashara ukilinganisha na manispaa ya kigoma ujiji.
Kasulu ni wilaya ambayo pia wanazalisha zao la
tangawizi kwa wingi ambapo ni zao la kibiashara hivyo watu kutoka mikoa
balimbali huja wilayani humu ili kujipatia zao hilo na kwenda kuuza sehemu
mbalimbali.
Vilevile kasulu kutokana na kuwa wilaya ambayo iko
mpakani ndiyo wilaya inayopokea wakimbizi kutoka nchini Kongo na Bundi ambao
wapo katika makambi ya Nduta na Mtabila wakiwa chini ya uangalizi wa serikili
ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania pamoja na hirika la kuhudumia wakimbizi
duniani UNHCR.
Mkoa wa kigoma umejaaliwa kuwa na maeneo mengi sana
yenye majini yanayo anza na herufi K jamboambalo hufurahisha pale mgeni anapo
fika mkoani humo na kutamburiwa na bbadhi ya maeneo hayo ni haya yafuatayo
vKamala
vKibirizi
vKakonko
vKibondo
vKinazi
vKasulu
vKahabwa
vKalenge
vKasaka
vKatubuka
vKaseke
n.k
Nazaleti ni moja ya sehemu ambayo
wageni wengi hushangaa pale wanapo ambiwa kuwa kuna sehemu inaitwa nazaleti
hivyo watu wengi hupenda kutembelea soko la nazaleti ikiwemo kununua vitu mbali
mbali sokoni hapo.
Manispaa ya kigoma ujiji imejaaliwa
kuwa na masoko mengi kwa mfano Mwanga senta, Buzebazeba,Kigoma marketi,Gungu
namengineyo ambapo watu wengi hupata mahitaji yao mhimu ya majumbani.
Ujijipia ni eneo la ki historia
ambapo inasadikika kuwa Dr. Living Stoni aliwahi kuishi lakini pia eneo hilo
limehifadhiwa kisheria hivyo watali hufika pale na kujionea manzali iliyopo.
Mawenin ndiyo hospitali ya mkoa
ambayo huhudumia wagonjwa wengi kutoka ndani ya manspaa lakini pia wilaya
zingine za mkoa huo huku hospitali ya Baptst ikiwa inaendeshwa na serikali hvyo
hupokea wagonjwa mbalimbali na wanapo zidiwa huhamishiwa maweni.
Jamanie kwa leo tuishie hapo ila
kumbuka kuwa haya ni baadhi ya mambo kati ya mengi yanayo patikana hukoo mkani
kigoma nilipata muda wa kufika mkoani hapo na kupita mtaa hadi mtaa ili kujua
kigoma kunani nikaona si vyema nikajua pekeyangu nikaona nikushirikise nawewe
msomaji wangu.
Nikushukuru kwa kuchukua muda wako
kusoma makala hiifupi lakini pia kama kuna lolote unaweza ukanitafuta kwa
mawasiliano yaliyop hapo chini na mimi sito sita kukujibu.
Namba. +255 713 305 650
Facebook. MC GOODLUCK
Email. Goodluckmc999@gmail.com


0 Maoni