NA.GOODLUCK CHRISTOPHER,
TULIISHIA HAPA
……..nasema tulia na kama ukijaribu kupiga kelele nakuchoma kisu
cha tumbo na kisha nijimalize namimi alisema kijana huyo.
#EPSODE-04
Kwa kitendo hicho Anitha alikosa namna ya kujinasua ilimbidi
kukubaliana na tendo lile ikizingatiwa kuwa tayari walikua na mapenzi ya siri
tangiapo shuleni wakayaanza misha ya
ndoa kwa namna hiyo.
Maisha mkoani Dodoma yaliendelea huku binti akaendelea
kudanganya anasoma na kuendelea kuomba pesa za ada na matumizi madogo madogo
pesa ambazo zilitumika kumsomesha mume wake pamoja na kula huku wazazi hawana
taarifa yakuwa mtoto wao aliolewa zaidi walijipa moyo anasoma.
Miezi kadhaa baadae Agness nae aliolewa katika kijiji cha
kazulamimba mkoani kigoma ambapo nae wazazi waliibariki ndoa hiyo basi aliishi
kwaamani na mume wake kama ilivyo kwa dada yake Vanesa alie olewa Morogoro.
Wazazi walifurahi sana kuona mabinti zao wawili kwenda kuanzisha
familia pamoja na kukuza ukoo jambo lililo wapa nguvu kundelea kutuma pesa kwa
Anitha kwani hawakujua kama Anitha amekwisha kuolewa .
Mwaka mmoja baadae Anitha alijifungua mtoto na wazazi wake
hawakupata taarifa yeyote juu ya jambo hilo zaidi waliendelea kutuma pesa
kwaajili ya matumizi kwa imani kuwa yupo Mwanza kimasomo kumbe yuko Dodoma
kindoa.
Basi siku hazingandi kijana aliingia mwaka wapili akiwa na
furaha kubwa kwa kuwa na mtoto pamoja na mke ambae anamuwezesha kusoma na
mapenzi yaliendelea kushamiri huku wakiwe wamekwisha kusahau yaliyo kwisha
kutokea kipindi cha nyuma kwani binti Anitha aliyapenda maisha yale.
Kijana alikaachini na kuona kuwa kuna haja ya kwenda
kujitamburisha kwa wazazi wa Anitha lakini ilimuwea vigumu akaona amshirikishe
amitha lakini iliwachukua muda kufikia mwafaka ya namna gani atafika kwa wazazi.
Basi mwafaka walio fikia ikaonekana kuwa kijana arudi pekeyake
akawaeleze wazazi na baadae wataenda wote mara baada ya kijana kujulikana
nyumbani kwa wazazi wa anitha,Mara safari ya kijana ilianza kutoka Dodoma
kuelekea katika kijiji cha katete Mkoani Kigoma.
Itaendelea……
N.B: Majina ya wahusika katika simulizi hii yemehifadhiwa
kwasababu za kiusalama kwasababu hili ni tukio la kweli ambalo lilitokea miaka
kadhaa iliyo pita hivyo nimeona si vyema kutumia majina harisi ya wahusika kwa
hilo nitaomba radhi msomaji wangu.
KWA MAHITAJI YA NAKALA YA SIMULIZI HII WASILIANA NA KITENGO CHA
MASOKO KUPITIA:
+255 713 305 650
KUPATA STORI,HABARI,ELIMU,BURUDANI NA DINI TEMBELEA MITANDAO
YETU IFUATAYO:
BLOG.planmediatz.blogspot.com
Facebook.PMTV_TZ
YouTube.PMTV_TZ
Instagram.pmtv_tz
Twitter.channel_plan
PLANMEDIA©2018


0 Maoni