NA,GOODLUCK CHRISTOPHER
Muimbaji wa nyhimbo za kumsifu Mungu /injili
Tanzania anaefahamika wajina la Ritha Komba amesema hajawahi kuwa kimya bali
anaendelea kuandaa kazi mpya, ameyasema mapema leo wakati akizungumza na PLAN
MEDIA TV.
Ritha ameieleza PLAN MEDIA TV Kuwa kwasasa
anaendelea kutengeneza video mpya unao itwa Nguvu yangu kwaajili ya kukamilisha
albam yake mpya inayo enda kwa jina la Rafiki inayo tarajiwa kuzinduliwa hivi
karibuni lakini kabla zindua albam hiyo ataachia video na audio ya Nguvu yangu.
Muimbaji huyo ametoa neon kwa wadau wa muziki wa
njili ndani na nje ya Tanzania kutoa kipaumbele kwa waimbaji na kutafuta namna ya kutoa nafasi kwa
waimbaji kufikisha nyimbo hizo kwa mashabiki ili kulifikisha neon kwa mataifa.
Ritha amemaliza kwa kuomba ushirikiano kutoka kwa
mashabiki wa muziki wa injili,maombi pamoja na maoni kutoka kwao ili aifanye
kazi ya Mungu.


0 Maoni