NA.GOODLUCK CHRISTOPHER,
TULIISHIA HAPA
Mara safari ya kijana ilianza kutoka Dodoma kuelekea katika
kijiji cha katete Mkoani Kigoma.
EPSODE-05
…… Mara safari ya kijana ilianza kutoka Dodoma kuelekea katika
kijiji cha katete Mkoani Kigoma.
Kijana akafika kijijini akamtafuta mzee mwenye busara kwaajiri
ya kwenda nyumbani kwa wazazi wa Anitha,
basi mzee yule alifika nyumbani kwa wazazizi wa anitha kwaajiri ya kuwajuza
ujio wa kijana huyo.
Mze huyo alipokelewa vyema nyumbani hapo kama mgeni japo wazazi
wa Anitha hawakujua kilicho mpeleka
nyumbani hapo basi alijitamburisha na kujieleza kuwa ;kuna jambo kubwa
limempeleka nyumbani hapo.
Wazazi wa anitha wakawa wanashauku kubwa yakujua ni jambo gani
lilikua limemleta mzee huyo “Wazazi wenzangu kubwa zaidi lilonileta hapa ni
jambo la kufurahisha sana kwani nimekuja kuwajulisha kuwa kijana wangu
amemchukua kijana wenu na anaishi nae kama mke na mume yapata miaka miwili
tangu waoane na cha kufurahisha zaidi wamebahatika kupata mtoto wakiume hivi
karibuni alisema mzee huyo.
Wazazi wa anitha wakaanza kushangaa na kutahamaki wa kumuuliza
mzee huyo ili kujua ni kijana yupi anamzungumzia kwakua wezee hao wanawatoto
wakike wapatao wawili ambao wamekwisha olewa, mzee ni mtoto gani huyo? Waliuliza
wa Anitha.
Basi mzee huyo alionesha tabasamu usoni mwake na kutaja Anitha,
Anitha? Waliuliza wazazi wa Anitha, Ndiyo Anitha alijibu kwa kujiamini mzee
Yule, Mbona mtoto wetu anasoma waliongea wazazi wa Anitha.
Nikweli kabisa wakati wanatoka hapa kijijini hawakuweka wazi
kama wanaenda kuoana lakini ukweli tokea siku zile yapata mika miwili wakiishi
kama mke na mume na siyo kusoma kama mnavyo dhani aliongea mzee yule.
Wemzee mbona unanivuruga lakini ebu ongea mambo ya maana na si
kuongea utani saizi aliongea Baba wa Anitha, Si muda wa kutaniana mzee
mwenzangu na hivi kijana amenituma kuja kuomba nafasi ili kesho aje
kujitamburisha aliongea mzee Yule.
Basi babayake na ndipo alimrarua ngumi za uso akadondoka chini
watu wakawahi kuja kuamua ugomvi ulie na kumuamlisha Yule mzee kwamba aondoke
na badala yake kijana mwenyewe aje wapate kuzungumza wote huku akiwa na jaziba
ya kufa mtu.
Mzee Yule aliamua kuondoka huku akiwa na maumivu makari
kutokana na kipigo alicho kipokea kutoka
baba Anitha alijikongoja mpaka kufika kwake kwani alikua hana jinsi ya kufanya.
Ikawa mzee alipo fika aliaamua kumweleza kijana kilicho mkuta
huko ndiupo kijana aliogopa sana kwamba endapo ataonekana mbele ya baba Anitha
kichwa chake kitakua harari yake.
Kijana hakutaka kuchelewesha mambo alikusanya kila kilicho chake
na usiku wa manane aliamua kutoroka na kuamua kurudi huko Dodoma huku akiwa na
woga mkubwa kwamba endapo akikutana na baba Anitha basi atakua amekwisha.
Wki moja baadae baba Anitha alipokea taarifa kuwa kijana
amekwisha kutoroka pasipo kuzungumza nae wala kumuona hivyo alipatwa na gadhabu
juu ya kijana Yule lakini alikua hana la kufanya kwa muda huo.
Basi kijana alikua amekwisha kurudi kwa mke wake huko Doma
akamweleza kilicho jiri huko basi Anitha
alipatwa na hofu kubwa moyo na kuwaza kwamba atarudi viupi nyumbani kwao.
Lakini pia kwa kijana huo ndio ulikua mwisho wa masomo yake
kwani alikua hana uwezo wa kujilipia ada ya mwaka mmoja uliokua umebaki maana
alikua anategemea mfuko wamkwewe.
Masha yakaanza kuwa magumu kiasi cha kukosa chakula ikizingatiwa
hawana kazi yeyote mjini inayo waingizia pesa basi wakaji change change na
miezi kadha baadae walifungasha vilago mpaka kijini kwao katete lakini
wakafikia nyumbani kwa wazazi wa kijana.
Wakati wakiendelea kutafakari ni jinsi gani wanaweza kwenda
kuomba msamaha kwa wazazi wa Anitha basi baba anitha alikua amekwisha kupata
taarifa kuwa wapo kijijini hapo.
Wiki kama mbili baadae alifanya upelelezina kujua wapi
walipondipo alipo muagiza mjumbe na kuwataka siku mbili baadae waweze
kufika nyumbani atakua na mazungumzo
nao.
Mjumbe Yule alipata kufikisha taarifa ile lakini wao hawakuweza
kutii wito ule na badala yake waliamua kuto kwenda wakihofia kwamba huenda akawadhuru.
Baba Anitha alichukia sana na zilipo pita wiki mbili na nusu
alimwagiza mjumbe wapili lakini bado pia
hawkuitika wito basi aliwachoka watoto wale.
Ikapita siku moja ndipo aliamua kuchukua uamzi mgumu wa kuandika
kwenye kaeatasi maneno yafuatayo “Katika mabinti zangu watatu ambao ni
Anitha,Agness na Vanesa kuanzia leo watafanikiwa mpaka washangae watoto
wafuatao Agness na Vanesa lakini namlaani mtotowangu nilemzaa Anitha pamoja na
mmewake kuanzia leo hawatokaa wafanikiwe kwa lolote mpaka kufakwake isipo kuwa
watakapo kuja kuniomba msamaha na kiasi cha pesa kisicho pungua milioni4 za
kitanzania pamoja na mbuzi mmoja nje na
hapo hawato fanikiwa daima na milele.“
Basi baada ya kuandika wakala huo akamuagiza mjumbe wa tatu aweze kuwapelekea
nae hakusita aliwafikishia Anitha alilia sana na kujutia alicho kifanya lakini
wahenga husema majuto ni mjukuu na maji yakisha mwagika haya zoeleki tena.
Paka leo hii Anitha anaishi maisha mabaya sana istoshe hana
uwezo wa kupata kiasi cha milioni 4 na istoshe hana kazi yeyote na Yule kijana
ni kama wametengana kutokana na ugumu wa maisha ikizingatiwa mtoto wao
anahitaji matunzo.
Nahuu ndio mwisho wa simulizi yetu hatimae Anitha ameishia
kulaaniwa kwa mambo aliyo jitakia
kupitia simulizi hii basi tupate kujifunza kitu.
USIKOSE SIMULIZI ZINGINE NZ NZURI ZINAZO KUJIA HIVI KARIBUNI
KUPITIA HAPA HAPA PLAN MEDIA.
MWISHO
N.B: Majina ya wahusika katika simulizi hii yemehifadhiwa
kwasababu za kiusalama kwasababu hili ni tukio la kweli ambalo lilitokea miaka
kadhaa iliyo pita hivyo nimeona si vyema kutumia majina harisi ya wahusika kwa
hilo nitaomba radhi msomaji wangu.
KWA MAHITAJI YA NAKALA YA SIMULIZI HII WASILIANA NA KITENGO CHA
MASOKO KUPITIA:
+255 713 305 650
KUPATA STORI,HABARI,ELIMU,BURUDANI NA DINI TEMBELEA MITANDAO
YETU IFUATAYO:
BLOG.planmediatz.blogspot.com
Facebook.PMTV_TZ
YouTube.PMTV_TZ
Instagram.pmtv_tz
Twitter.channel_plan
PLANMEDIA©2018


0 Maoni