NA. GOODLUCK
CHRISTOPHER
Kwa mara nyingine tena plan media
inakuletea makala yenye mafundisho ya hali ya juu lengo likiwa ni kila
mtanzania kupata elimu juu ya mabo ambayo hayajui na kama anayajua basi
tunamuongezea maarifa chamsingi ni kuhakikisha hupitwi na kitu kwa kutembelea planmediatz.blogspot.com
kila siku.
Na
makala ya siku ya leo tumeamua kuwaletea suala nyeti sana ambalo watu wengi
hawalielewi kiundani hivyo pasipo kupoteza muda niovyema nika kukaribisha
kuchukua muda wako kusoma makala hii kwa umakini na Kama kuna sehemu huelewi
basi uta uliza kwa kukoment hapo chini.
Swali
linalo gonga vichwa vya watu ni je mimba za utototoni ni nini?
Kiukweli hapa
kila mtu anajibu lak analo lifikilia kutokana na uelewawaalio nao ili ni jambo
lisilo pingika kwamba mimba za utotoni ni ule ujauzito unaopatikana kwa mtoto
wakike akiwa chini ya umri wa miaka 18.
Kwa
mjibu wa taasisi na mashirika mengi duniani yanayo tetea haki za watoto mimba
za utotoni zinapigwa vita na watetezi hao kwa dhana kwamba ni noja wapo ya
unyanyasaji wa kijinsia kwa watoto nah ii ni ukweli kwamba suala hili ni ukweli
usio pingika kwamba ni ukatili wa hali ya juu kwa mtoto chini ya umri wa miaka
18.
Daaaah!!!
Swali ambalo huwa najuliza na likawa linaniumiza kichwa ni je, ni kwani mimba
za utotoni zinatokea jeee? Hapo nilikua nawaza kwa sauti na wala sikupata jibu,
baada ya kukosa jibu unajua nilifanya kitu gani? Hahahaha!!! Ebu angalia
nilicho kifanya.
Aiseeeeee!
Nimegundua utafiti ni kitu kizuri sana na ndo maana napenda sana kufanya
utafiti basi msomaji wangu niliamua
kupita mta kwa mtaa nikihoji lengo nikitaka kujua kwanini mimba za
utotoni zinatokea? Basi mtaani ilikua hivi:
Ø Utandawazi
Ø Tamaa za watoto wenyewe
Ø Malezi
Ø Mila na Tamaduni
Ø Umasikini
Na
hivyo ndivyo ilivyokua mtaani watu waliweza kufunguka vile vyenye wanaelewa
lakini si kuishia hapo niliamua kuhoji kwa kina kujua vitu hivyo vinasabisha je hizo mimba unajua
ilikuaje? Usijali nilifuatilia kwa kina ikawa hivi:
UTANDAWAZI
Basi
neon hili lina maana nyingi kama nini mimi nikaamua kuchukua neon hili
mabadiliko katika Nyanja mbalimbali katika maisha ya kibinadamu kwamfano
mawasiliano nimetumia mfano huu lakini kuna vingi vinavyo fanana na hilo.
Utandawazi
ni kitu ambacho kinachangia watoto kujihusisha na na mitandao ya kigono kingali
wadogo na wanapo jaribu tu kujiingiza katika tendo lisilo takatifu la ndo
hujikuta wamezama na matokeo yake huwa ni kuambulia kubeba ujauzito chini ya
umri wa miaka 18.
TAMAA
ZA WATOTO WENYEWE
Uuuuuuuuuuuwi!!
Hapa sasa nilipata utata ila nilipata kuchagua jibu moja kati ya mengi nalo ni
baadhi ya vijana wanaonekana kutomani vitu wasivyo navyo ili kukidhi mahitaji
yao madogomadogo ambayo hawayapati katika familia zao mfano. Zawadi ndogondogo
kutoka kwa mwanaume kama chips mayai, kutolewa out yani katika maeneo ya
starehe, Lifuti, Simu na vocha zake na vitu vingine kama hivyo.
Basi
iko hivi sikuzote ukila utaliwa kimsingi iko hivyo na siku zote wahenga husema tama
mbaya hivyo matunda ya kutamani huwa ni kuambuliamatatizo kwa mantiki hiyo basi
mabinti wengi hujikuta wakitumbukia kwenye dimbwi la mimba kingali watoto.
MALEZI
Malezi
ni suala pan asana hivyo wakati nikipita mtaa mpaka mtaa nilipata kupewa maana
nyingi za neon hilo ila kwa leo naomba tutumie hii hapa. Ni yale mafundisho na
maonyo ambayo mtoto hupewa kutoka kwa wazazi ama walezi wa mtoto huyo.
Basi
wahenga husema mtoto umleanyo ndivyo akuavyo kwa mantiki hii wazazi wengi
wamekua wakilia watoto wao vibaya ikiwemo kuwapa uhuru ulio pitiliza jambo
linalo wafanya watoto wengine kuwa na tabia mbaya ambayo hupelekea watoto wengi
kujisahau na kujiingiza katika dimbwi la mahusiano ya kingono kingali wadogo
hali inayo pelekea kubeba ujauzito chini ya umri wa miaka 18.
MILA
AU TAMADUNI
Haya
ni masuala ya mambo yanayo fanya na asili moja ya watu wanao fanana kwamfano
ukoo,kabira au inaweza kuwa hata taifa hivyo mambo haya huchangia mimba za
utotoni katika baadhi ya makabira katika nchi yetu ya Tanzania au bara la
Afrika kwa ujumla.
Kwa
baadhi ya makabira mfano wasukuma,wakurya,wamaasai nawewengine kama hao kwa
kipindi cha nyuma waliongoza sana katika mimba hizo za utotoni richa ya
serikali na wadau mbalimbali kupiga vita sula hili kwani wao waliamini
kumuozesha binti mapema huongeza heshima ya ukoo wao pamoja na kujipatia mifugo
kutoka kwa muoaji.
UMASIKINI
Niile
hali ya binadamu kukosa mahitaji mhimu ambayo binadamu anastahili kupata
kwamfano pesa,chakula,mavazi pamoja na malazi na vitu vingine kama hivyo hii
ndiyo dhanaya umasikini na mtu anapo kosa vitu hivyo basi anapaswa kuitwa
masikini.
Nikweli
kabisa kwamba binadamu ili akamilike lazima apatemahitaji yake yamhimu hivyo
basi kwa mtoto wa lkike anapo kua amekosa mahitaji yake nyumbani basi huamua
kutafuta ama kuombaomba kwa wanaume ili kukidhi haja zake kwa Kiswahili cha
vijana waleo wanasema kudanga jambo
ambalo huwapelekea kubeba ujauzito kwasababu hukosa vya kuwalipa walio wapatia
vitu hivyo na kuamua kulipa utu wao.
Jamanie
hayo ni baadhi ya ambayo nimeyapata huku mitaani ama uswazi uswahilini kusema
kweli uswahilini kuna vituko ten asana lakini swali la kujiuliza mimi nawewe ni
je suruhilo la hili ni lipi? Usijali bado nipo huku uswahilini pengine ngoja
niendelee kuhoji harafu tuchangie kitakacho patikana.
SURUHISHO.
Msomaji
wangu kila chenye mwanzo hakikosi mwisho nimejaribu kuhoji sana na kupata
majibu mengi na moja katka hayo ni haya hapa yafuatayo.
Ø Kutoa elimu ya jinsia kwa watoto
Ø Kuwa karibu na watoto wetu
Ø Matmizi bora ya utandawazi
Ø Kuridhika na kipato cha mzazi wako
Ø Kuacha nila na tamaduni potofu
Ø Kuacha tama
Ø Malezi bora kwa watoto
Hayo
yalikua ni baadhi yamambo yanayo paswa kuzingatiwa zaidi ili kujiepusha na
mimba za utotoni lakini ikumbukwe kuwa mimba za utotoni huharibu taifa kwani
hukatisha ndoto ya mtoto jambo ambalo hupelekea kuwa na wanchi wajinga hivyo
tuchukue tahadhali mapema kabla haya jatukuta.
Ebanaeee
kutoka huku uswazi uswazini maarufu kama mtani kwetu kwa leo sinala ziada hivyo sina budi kurudi mitamboni pale mitaa
ya ilala bungoni kuwasirisha kile nilichokipata huku mtaani lakini pia tukutane
kwenye makala nyingi sana zinazo kuja hivi karibuni naitwa GOODLUCK CHRISTOPHER
Nitafute kwa mawasilianoyafuatayo
Facebook.
MC GOODLUCK
Contact.
+255713 305 650



0 Maoni