NA.GOODLUCK CHRISTOPHER,
TULIISHIA HAPA.
…………… hivyo wazazi walijikusanya na kumpatia pesa kwaajiri ya kumpeleka shule.
#EPSODE-03
Baada ya wazazi kujikusanya walimkabidhi kiasi cha milioni moja
za kitanzania ndipo walipanga safari binti akijua wanaelekea chuoni huko mwanza
lakini haikuwa hivyo kwa mwanaume Yule na kwavile Anitha alikua hajui njia
yakwenda huko mkoaniMwanza alimsikiliza mwanaume alikua anafuata njia anayopita
mwanaume yule.
Wakapanda gari moshi kuelekea mkoani Dodoma kwa makubaliano
yakuwameoana lakini mwanaume akiwa ameenda kusoma chuo cha St. Joseph tawi la
Dodoma katika taaluma ya Ualimu wakati huo binti Anitha alikua hajui chochote
kuhusu hilo kwani mwanaume Yule hakumdokeza maana alijua akimdokeza lengo lake
halita kamilika.
Ikawa walipo fika Dodoma mwanaume akachukua ile pesa na
kumweleza Anitha kuwa hawato weza kwenda mwanza na hawezi tena kusoma na badala
yake pesa hiyo itatumika kumsomesha yeye na si Anita kama ilivyo tarajiwa.
Kutokana na ugeni wa mji lakini pia kuchukuliwa pesa na simu
yake Anitha alichanganyikiwa na kwa muda huo hakujua ajiokoe vipi katika
mazingira hayo hivyo siku nzima alikua ni kama mtu ambae hajitambui ilimbidi
kuwa mpole huku akisubiria kitakacho endelea.
Ikafika usiku ndipo Anitha alishangaa kuona anapelekwa
chumbani kwaajili ya kulala huku akijua
kuwa kijana atakua ametafuta chumba kingine cha kulala lakini haikuwa hivyo
kijana alimuamru kulala kitanda kimoja na kumweleza wazi kuwa amemuoa.
……nisikilize Anitha sikuzote nimekua nikitafuta njia ya kuishi
nawewe lakini nimekua sipati nafasi hiyo hivyo najua leo hii hauna ujanja
utakua mke wangu kuanzia leo mpaka pale kifo kitakapo tutenganisha alisema
kijana huyo.
Anitha alilia sana huku akitaka kutoroka chumbani pale lakini
kijana alimshikia kisu na kutaka kumchoma……..nasema tulia na kama ukijaribu
kupiga kelele nakuchoma kisu cha tumbo na kisha nijimalize namimi alisema
kijana huyo.
Itaendelea……
N.B: Majina ya wahusika katika simulizi hii yemehifadhiwa
kwasababu za kiusalama kwasababu hili ni tukio la kweli ambalo lilitokea miaka
kadhaa iliyo pita hivyo nimeona si vyema kutumia majina harisi ya wahusika kwa
hilo nitaomba radhi msomaji wangu.
KWA MAHITAJI YA NAKALA YA SIMULIZI HII WASILIANA NA KITENGO CHA
MASOKO KUPITIA:
+255 713 305 650
KUPATA STORI,HABARI,ELIMU,BURUDANI NA DINI TEMBELEA MITANDAO
YETU IFUATAYO:
BLOG.planmediatz.blogspot.com
Facebook.PMTV_TZ
YouTube.PMTV_TZ
Instagram.pmtv_tz
Twitter.channel_plan
PLANMEDIA©2018


0 Maoni