NA.MWANDISHI WETU
Makamu wa rais wa Botswana, Mokgweetsi Masisi,
ameapishwa kama rais katika sherehe iliyofanywa mji mkuu, Gaborone.
Masisi, ameshika hatamu kutoka kwa Rais Ian
Khama, ambaye aliondoka madarakani jana, baada ya kuongoza kwa miaka 10.
Botswana itafanya uchaguzi mwaka ujao.Botswana
ni ya pili kati ya nchi zinazochimba almasi nyingi kabisa.
Baada ya kuapishwa, Rais Masisi, alisema kuwa
kupunguza ukosefu wa ajira kati ya vijana, ndio jambo muhimu kabisa kwake, na
pia aliahidi kuyapa kipa-umbele, mapambano dhidi ya Ukimwi, utumizi mbaya wa
ulevi na madawa ya kulevya, pamoja na rushwa.
SOURCE.BBCSWAHILI.COM
0 Maoni