NA.GOODLUCK CHRISTOPHER,
TULIISHIA HAPA.
……… Nitalima tu wakati nikisubiria kuolewa, Basi wazazi
walijitaidi kumshauri lakini binti alikataa kusoma dipo waliamua kumwacha
achague alicho chagua.
#EPSODE-02
Siku zilienda na hatimae binti akapata mume akaolewa mvomero
huko mkoani Morogoro na maisha yaliendelea akiwa huko na wazazi wakabariki ndoa
hiyo lakini wakati huo Anitha alikua kidato cha tatu ambapo Agness nae alikua
amekwisha maliza darasa la saba nae pia alikataa shule hivyo wazazi wake
hawakuumiza kichwa walimwacha tu zaidi waliongeza nguvu kwa Anitha maana
waliipenda ndoto yake.
Pindi Anitha anaendelea na masomo yake aliendelea kubadilika
taratibu kitabia mara baada ya kuanza mapenzi ya kisirisiri na mwanafunzi
mwenzie ambae alikua akiendelea kumlagai kwa kumpa vitu vidogo vidogo akajikuta
amezama jambo ambalo lilimfanya ashuke kitaaluma akaanza kufanya vibaya
darasani lakini familia haikupata kujua hayo kwani walimuamini mtoto wao kwa
asilimia 100% istoshe wazazi wake hawakusoma
hivyo ilikua ni vigumu kukagua maendeleo ya mtoto wao.
Siku hazingandi Anitha
alihitimu kidato cha nne na kurudi nyumbani kusubiria matokeo yake na kumkuta
mdogo wake akiwa nyumbani hivyo maisha yakaendelea huku wazazi wakisubiria kwa
hamu matokeo yake ya kuendelea na kidato cha tano hatimae chuo kikuu.
Wakati akisubiria matokeo aliendelea kujihusisha na mahusiano ya
kimapenzi na vijana wa kijijini hapo kwani alikua amesha kuwa na sugu lakini
wazazi walipo pewa taarifa za binti yao hawakuamini zaidi waliona ni wivu wa
watu wa kijijini hapo juu ya mtoto wao hivyo basi hii ilimlinda sana mtoto
huyo.
Baadae kidogo matokeo yakatangazwa ikaonekana matokeo yake siyo
mazuri ambapo alipata [FOUR YA 30] ambapo kwa kawaida ailionekana hana sifa za
kuendelea na kidato cha tano wala chuo chochote cha ufundi isipo kuwa VETA,
Lakini pia kijana ambae walikua na mahusiano nae shuleni alipata [FOUR YA28]
Ambapo ilionekana kuwa anasifa za kujiunga na vyuo vya vya kati.
Basi kijana ilionekana kwao hakuna pesa ya kumsomesha ndipo
aliunda mbinu ya kumlagai Anitha kwamba akawadanganye wazazi wake kuwa kuna
chuo kimepatikana mkoani mwanza kinapokea wanafunzi mwenye FOUR YA 32 Katika
taaluma ya afya yaani Nursing hivyo wazazi walijikusanya na kumpatia pesa
kwaajiri ya kumpeleka shule.
Itaendelea……
N.B: Majina ya wahusika katika simulizi hii yemehifadhiwa
kwasababu za kiusalama kwasababu hili ni tukio la kweli ambalo lilitokea miaka
kadhaa iliyo pita hivyo nimeona si vyema kutumia majina harisi ya wahusika kwa
hilo nitaomba radhi msomaji wangu.
KWA MAHITAJI YA NAKALA YA SIMULIZI HII WASILIANA NA KITENGO CHA
MASOKO KUPITIA:
+255 713 305 650
KUPATA STORI,HABARI,ELIMU,BURUDANI NA DINI TEMBELEA MITANDAO
YETU IFUATAYO:
BLOG.planmediatz.blogspot.com
Facebook.PMTV_TZ
YouTube.PMTV_TZ
Instagram.pmtv_tz
Twitter.channel_plan
PLANMEDIA©2018


0 Maoni