NA.GOODLUCK CHRISTOPHER,
Hii ni simulizi ya kweli iliyo tokea katika kijiji cha Katete
Kata ya Mwakizega Mkoani Kigoma ambayo inamhusu Binti anae fahamika kwa jina la
Anitha ambae alipata laana kutoka kwa baba yake mzazi tafadhali fuatilia kisa
hiki.
Nikukaribishe msomaji
wangu katika simlizi hii fupi yenye kusisimua na mafundisha kwa jamii kutokana
na mambo yanayo tokea katika familia zetu.
Kabla ya kuianza simulizi yetu tuanze na kumfahamu mhusika wetu.
Anitha ni binti alie zaliwa katika kijiji cha Katete huko uvinza mkoani kigoma
na ni mtoto wa kwanza katika familia yenye watoto sita huku watoto watatu
wakiwa ni wakike na wakiume wakiwa ni watau pia kuanzia mtoto wakwanza mpaka wa
tatu wote ni watoto wa kike kwa maana hiyo familia hii ilipata watoto wa kiume
mwishoni kama mwenyezi Mungu alivyo panga.
EPSODE-01
[WOSIA WA WAZAZI]…..Mwanetu
tunakupeleka shule ili uje kuwa mwokozi wa familia yetu maana tumechoka na huu
umaskini walisema wazazi wa Anitha wakati akiwa shule ya msingi Katete, Msijali
wazazi wangu kwasababu ndoto yangu ni kuwa Daktari mkubwa tena wa kimataifa na
nitakununulieni gari kila mmoja wazazi wangu lakini pia nitawajengea nyumba
nzuri tena ghorofa yenye bwawa la kuogelea hapa nyumbani alisema Anitha.
Tunafurahi
sana mwanetu tunashukuru kwakua unafahamu umhimu wa kusoma na sisi tutafanya
juu chini usome mpaka uitimize ndoto yako walisema wazazi wake.
Wazazi wa Anitha walikua ni wakulima wadogowadogo wanao tumia
jembe la mkono hivyo waliongeza ukubwa wa mashamba lengo ikiwa ni kuhakikisha
mtoto wao wanamtimizia ndoto yake na haki yake ya msingi ya kupata elimu na
kumbuka kuwa wakati huo wadogo zake wawili walikua nao wamekwisha kuanza shule
basi hata mahitaji yao yaliongezeka zaidi kutokana nakua wanafunzi walikua ni
watatu hivyo wazazi walilazimika kununua sale,madafutari na ada ya Anitha
pamoja na wadogo zake wawili ambao ni Vanesa na Agness.
Basi Anitha alihitimu masomo yake ya msingi na kufaulu vizurina
kufanikiwa kujiunga na kidato cha kwanza
ambapo wazazizi wake walimpeleka kidato cha kwanza katika shule ya
Luchugi Secondary School iliyopo huko uvinza mkoani Kigoma wazazi walifurahi
sana kwa kuona mtototo wao kuendelea kupiga hatua hususa ni pale wakiikumbuka
ahadi ya mtoto wao.
Basi Anitha aliendelea na masomo yake na alionekena mwanafunzi
anae fanya vizuri darani lakini wakati huohuo wadogo zake walionekana kuto
ipenda shule wakiwa bado wako shule ya msingi na kipindi Anitha amefika kitato
cha pili mdogo wake Vanesa alihitimu elimu yake ya msingi na kufaulu lakini
alikata kuendelea na elimu ya sekondari.
……..Nawaombeni msijisumbue kunipeleka kujiunga na kidato cha
kwanza sijisikii kuendelea na kama mkinipeleka shule basi nitakula pesa zenu tu
na sitokaa darasani hata siku moja alisema Vanesa akiwaambia wazazi wake, Sasa
wewe unataka nini? Walimuuliza wazazi wake, Nitalima tu wakati nikisubiria
kuolewa, Basi wazazi walijitaidi kumshauri lakini binti alikataa kusoma dipo
waliamua kumwacha achague alicho chagua.
Itaendelea……
N.B: Majina ya wahusika katika simulizi hii yemehifadhiwa
kwasababu za kiusalama kwasababu hili ni tukio la kweli ambalo lilitokea miaka
kadhaa iliyo pita hivyo nimeona si vyema kutumia majina harisi ya wahusika kwa
hilo nitaomba radhi msomaji wangu.
KWA MAHITAJI YA NAKALA YA SIMULIZI HII WASILIANA NA KITENGO CHA
MASOKO KUPITIA:
+255 713 305 650
KUPATA STORI,HABARI,ELIMU,BURUDANI NA DINI TEMBELEA MITANDAO
YETU IFUATAYO:
BLOG.planmediatz.blogspot.com
Facebook.PMTV_TZ
YouTube.PMTV_TZ
Instagram.pmtv_tz
Twitter.channel_plan
PLANMEDIA©2018


0 Maoni