Habari ndugu msomaji na mpenzi wa Plan Media natumaini umzima waafya na kama hujisikii vizuri kiafya Mungu alie juu akupe afya njema ili uweze kupata nguvu na kuweza kuendelea kupata vitu vizuri kupitia media yako uipendayo, nikukaribishe ndugu msomaji katika kusoma makala hii fupi ambayo itakupa maarifa zaidi kuhusu kipaji nisikuchoshe msomaji wangu twende moja kwa moja kwenye maana harisi ya neno kipaji.
KIPAJI NINI?Kipaji ni uwezo waasili wa kufanya jambo fulani au ni uwezo ambao mtu amezaliwa nao wa kuweza kufanya jambo fulani, tunapo zungumzia kipaji nitofauti na mtu ambae amepandikizwa uwezo wa kufanya jambo fulani kwa maana ya kufundishwa kufanya jambo hilo lahasha mtu mwenye kipaji hufanya jambo hilo kwa uwezo wa asili aliopewa na Mungu.
Kila mtu huwa anaelezea vile anavyo elewa juu ya neno hili la kipaji pengine wewe utakua una maana yako juu ya neno hili ila nivizuri tukatumia maana moja tu katika makala hii fupi ili tuweze kuelewana wote kwani nikitumia maana nyingi zaidi nitakuchanganya wewe msomaji wangu wa makala hii.
Kuna aina nyingi sana za vipaji ambavyo watu wanavyo ama wemejaliwa na mungu tangia walipo zaliwa kwamfano:, Kuimba, Kucheza, Kuigiza,Kucheza mpira,Kujenga, Kuchora,Kuchonga,Kufundisha,Uandishi, Utangazaji,Ususi n.k.
Ikumbukwe kuwa kila binadamu alie ubwa na Mungu anakipaji chake ambacho alijaliwa tangia kuzaliwa kwake pengine unaweza ukaona kwamba kuna baadhi ya vipaji sijavitaja ila ukweli nikwamba kuna vipaji vingi mno kwa leo naomba nikutajie hivyo na Mungu akijalia nitaanda makala nyingine ndefu ambayo nitaongeza mifano ya vipaji ambavyo sijavitaja katika makala hii endelaea kusoma hapo chini kuhusu kipaji.
Tunapo zungumzia vipaji kuna watu ambao hawaelewi kuwa wao wana vipaji gani pengine limekua ni tatizo kubwa kwani usipojua kipaji chako utakua unalazimisha kufanya kitu ambacho si kipaji choko napengine unaweza usifanikiwe kwasababu utakua unajilazimisha kufanya kitu usicho kiweza hivyo ni mhimu kujua kipaji chako ni kipi.
Je,kipaji chako ni kipi?
Swali hili linaweza kuwa ni gumu ama jepesi ila nivizuri uka comment kipaji chako hapo chini itakua vizuri zaidi kwani kunawatu huwa wanashindwa kujibu swali la mhimu katika maisha tunayo ishi ya kila siku kwa sababu kuna umhimu wa kujua kipaji chako kwani kipaji chako ni mafanikio yako.
Kuna watu ambao wamebahatika kujua vipaji vyao ila wanashindwa kuvitumia ama kufaidika navyo hili limekua ni tatizo kubwa ambalo lina wakumba watu wengi na hasa wa afrika katika nchi za wenzetu wazungu huwa wanajali sana vipaji tofauti na sisi wa afrika kwakua wazungu wao huwa wananza kuvilea na kuvikuza tangia utotoni na ndiyo maana katika nchi zao zina maendeleo makubwa na mtu huwa anafanya shughuli kulingana kipaji alicho jaliwa na Mungu tofauti na sisi wa afrika ambao hatufatilii sana kuhusiana na vipaji japo ku baadhi wanajitahidi kukuza na kulea vipaji mbalimbali kwa kuanzisha taasisi zinazo jishughulisha na vipaji hili ni jambo la kumshukuru Mungu kwa watu hawa kutambua hilo japo juhudi na elimu kwa jamii zinahitajika kwa sana ili kulielewa hili.
Kunawatu ambao wanajitambua kuwa wanavipaji na kuvitumia ila huwa hawafaidiki na vipaji vyao zaidi wanawafaidiasha wengine ambao hawana vipaji hivyo, unaweza usinielewe ila wewe mwenyewe ni shahidi niwatu wangapi? wanaokuzunguka ambao wanavipaji na wabunifu wa hali ya juu ila hawafaidiki navyo pengine hatawewe msomaji wa makala hii huenda hufaidiki na kipaji chako ila hujachelewa haijalishi una umri gani chamsingi ni kujitambua una kipaji gani? kupitia makala hii unaenda kufanikiwa kupitia kipaji chako.
Kuna watu maalumu ambao wapo na wana mafanikio makubwa lakini mafanikio yao siyao bali kupitia vipaji vya wengine pengine wewe kuna mtu unamfaidisha kupitia kipaji chako kwa kujua au pasipo kujua hii unaweza usinielewe labda nikuulize swali kipaji chako toka ujitambue kama unacho umefaidika nacho vp? Hili ni swali jepesi na gumu sana lakini swali jingine hakuna anae faidika zaidi yako kupitia kipaji chako? Majibu ya maswali hayo ebu comment hapo chini na kiasha tuendelee na makala hii kwani lengo la makala hii ni ufaidike na kipaji chako.
Ni makosa makubwa sana kutumia kipaji cha mwingine kama mtaji kwani ukifanya hivyo utakua unamkosea Mungu alie mpa kipaji hicho na ukiona mwenzako ana kipaji na hatambui kama anacho ni vizuri ukamweleza kipaji chake na kimfundisha pia jinsi ya kufaidika nacho.
Pale unapogundua kipaji chako ni kipi usikubali mtu ueyote aweze kukutawala juu ya kipaji chako ni mhimu kuwa mtetezi wa kipaji chako kwani utakapo kubali kutawaliwa juu ya kipaji chako utaiashia kuwa nacho na hautakifaidika nacho mpaka kufa kwako.
PLAN MEDIA tumegundua umhimu na kuthamini vipaji vya aina zote hivyo kama una kipaji chochote ni mhimu ukawasiliana nasi kwa namba nitakazo wawekea hapo chini kidogo, tumejipanga kutoa elim na kuvitangaza vipaji vya watu leongo ikiwa ni kila mtu kufaidika na kipaji alicho jaliwa na Mugu.
Mawasiliano:
Tell no. +255 713 305 650
Email. planmediatz.@gmal.com
Instagram. planmediatz
Nakumbuka miaka ya 90 kulikua na masomo maalumu mashuleni ambayo yalikua yanahusu maswala ya vipaji ambayo kwa hivi sasa hayatiliwi mkazo na ndiosababu kubwa ya watu wengi kushindwa kutambua,kutumia na kufaidika kwenye vipaji vyao kwani wanavitambua kuwa wanavyo ukubwani wakati umri umesha enda hivyo inakua ngumu kufaidika navyo ila kupitia Plan Media utafaidika nacho tu.
Kama unavyoona pichani ni mmoja wa watoto wa ki afrika ambae ana kipaji cha pekee cha kutengeneza ramani za nyumba kama unavyoona pichani kwa wa afrika wanavyo penda kupuuzia vitu mtu anapokua na mtoto mwenye uwezo wa kuunda kitu kama hicho wanamuona wa kawaida ila mtoto huyo anakitu kizuri sana ndani yake mtoto kama huyu katika nchi za wazungu anathaminiwa sana tofauti na sisi wa afrika kwakua watu kama hawa wanakua ni wabunifu na wachoraji wa ramani za majengo makubwa kama ma ghorofa.
Tunao watu wengi kama huyu na si kwa kipaji hiki tu na vingine pia ila thamani yao haipo kwenye jamii utakua ni shahidi wa hapo mtaani kwako unapoishi kuwa wapo wangapi wa aina hii? Jibu la swali hili kwa kucoment hapo chini.
Kuna faida nyingi sana unapo tumia vizuri kipaji chako ipasavyo kwakua tumewaona wengi wakifadika na vipaji vyao muda nisasa kipaji chako mafanikio yako jaribu kuwaailiana nasi au kututembelea tunapatikana Dar es salaamTanzania,tumejipanga kuhakikikisha unafanikiwa na kipaji chako mawasiliano ndo hayo hapo juu.
Huu ndo mwisho wa makala hii fupi iliyokua inahusu vipaji, nikushukuru wewe ulie soma mwanzo mpaka mwisho naamini umejifunza kitu endelea kutembelea media yetu kwani tumejipanga kukuletea vitu vizuri sana na uvipendavyo usichoke kutembelea media yetu na kusamba taarifa kwa wengine.
Makala hii imeandaliwa,kuhaririwa na Mc Goodluck.
Je,Wewe ni Msanii au Mfanya biashara? Na unapenda kutangaza na Plan Media ? Jibu kama nindio piga simu namba 0713305650 tukutangazie tangazo lako kwebei nafuu ambayo haijawahi kutokea.
Tembelea mitandao yetu ambayo ni.
Blog. @planmediatz.blogspot.com
YouTube. @PLAN TV ONLINE
Facebook. @planmediatz
Instagram.@planmediatz
@planmedia2017

2 Maoni
Yeah kwa wale wengi hawakufahamu kuajipaji ni nini hasa tayari hapo ushapata kufamu na kuelewa vyema kuhusu kipaji Mimi kama MSANII wakuimba na shukuru Mungu sana kwa hilo kipaji alio nipa nducho cha niongoza maeneo yote nayo enda asante Mungu kwa kipaji. Sheshee man.
JibuFutaChapisho hili limeondolewa na msimamizi wa blogu.
JibuFuta