LONDON/UINGEREZA.
Ligi Kuu ya soka ya England ndiyo yenye kutazamwa na watu
wengi zaidi kuliko yoyote ile duniani. Ndiyo tajiri zaidi kulizo zote ikiwa
imeweza kuvutia wachezaji bora kutoka kila pembe ya dunia. Lakini ni ngumu
kuamini kwamba mpira ya kwanza kupigwa katika Ligi Kuu ya Premier ilikuwa hivi
karibuni tu 15 mwezi wa Nane 1992.
Kipindi cha miaka ya 1980 kilikuwa kigumu kwa soka La
Englan,Uhuni katika viwanja vingi vya soka ulishamiri.Timu za soka za
England zilipigwa marufuku katika miuchuano ya Ulaya kufuatia vifo vya
mashabiki 39 katika uwanja wa Heysel nchini Ubelgiji kabla ya pambano la
fainali ya kombe la Ulaya kati ya Liverpool na Juventus mwaka 1985. Ni
wachezaji wachache bora duniani wangeweza hata kufikiria kucheza soka la
kulipwa England.
Ndipo mwaka 1989 ikatoka ripoti ya Hillsborough and the
Taylor. Washabiki wa soka 96 walifariki na wengine 150 walijeruhiwa katika
mechi ya nusu fainali ya Kombe la Chama cha Soka England (FA) kati ya Liverpool
na Nottingham Forest. Ripoti ya Lord Taylor ikapendekeza kubadilishwa kabisa
mfumo wa uendeshaji wa viwanja vya soka na kusababishwa kuanzishwa kwa
utaratibu wa kukaa vitini kwa watazamaji wote wa soka wawapo viwanjani.
Gharama kubwa za kutekeleza mapendekezo ya tume na hali ya
kutoweza kuvutia wachezaji bora wa kulipwa ikasababisha vilabu vikubwa kuonesha
hali ya kutoridhia, Mapema mwaka 1988, vilabu kumi vilitishia kujitoa kutoka Ligi
Kuu ili vifaidi mapato makubwa yatokanayo na matangazo ya runinga.
Hakika badiliko kubwa la muundo lilikuwa linahitajika ikiwa
klabu za England na mchezo wenyewe wa soka vilihitaji kustawi. Makubaliano ya
wanachama waanzilishi yakasainiwa 17 mwezi wa Saba 1991 na kuweka kanuni za
msingi za kuanzisha Ligi Kuu ya Soka. Ligi hiyo ingekuwa na uhuru wa kibiashara
toka kwa Ligi ya Soka na Chama cha Soka (FA), ikiwa na mamlaka ya kuratibu
mikataba yake yenyewe ya utangazaji na udhamini wa soka.
Tarehe 20 mwezi wa Pili 1992 klabu za ligi daraja la kwanza
zikang’atuka toka Ligi ya Soka kwa pamoja na miezi mitatu baadae Ligi Kuu ya
soka (Premier League) ikaanzishwa kama kampuni (limited company).
Ligi hiyo ikaamua kuchukua hatua kubwa kwa kuto haki za
matangazo ya runinga kwa kituo cha Sky TV. Wakati huo kutoza wapenzi wa soka
gharama za kutazama soka ilikuwa ni dhana mpya. Lakini ubora wa soka
uliotarajiwa kupatikana na mikakati mizito ya kutafuta soko ya kituo cha Sky
vikasababisha thamani ya Ligi ya Premier kukua. Makubaliano ya mwanzo yalikuwa
kiasi cha pound milioni 191 kwa kipindi cha miaka mitano.Kutangaza mechi za
soka kutoka 2007-2010 Sky na Setanta wamelipa kiasi cha pound bilioni 1.7!!
Udhamini pia umeweza kuwa na mchango mkubwa. Mwaka 1993
Carling ililipa pound milioni 12 kwa kipindi cha miaka minne na mashindano
yakajulikana kama FA Carling Premiership. Wakaongeza mkataba kwa miaka mingine
minne kwa ongezeko la asilimia 300. Mwaka 2001, Barclaycard wakawa ndiyo
wadhamini wapya na kutoa kiasi cha pound milioni 48 kwa kipindi cha zaidi ya
miaka mitatu. Barclays wakachukua udhamini mwaka 2004 na mwaka 2007 wakaongeza
bei kufikia pound milioni 65 kwa misimu mitatu.
Kuongezeka kwa mapato kumehakikisha kuwa timu za England
zinaweza kushindana katika ngazi ya dunia juu ya suala la ada za uhamisho wa
wachezaji na mishahara yao. Hii ni sababu kubwa ambayo imefanya baadhi ya
wachezaji wakubwa duniani kuing’arisha Barclays Premier League.
Mwaka 1992 kulikuwa na wachezaji 11 tu wasiokuwa waingereza
au wa-Irish katika Premier League. Kufikia 2007, idadi ikaongezeka na kufikia
250. Katika miaka yote hii wachezaji toka nje ya Uingereza wamechangia
kuing’arisha soka ya Uingereza. Makocha (meneja) kutoka nje pia wamekuwa pia na
shauku ya kufanya kazi England. Mbinu za ufundishaji wa soka za makocha kama
Arsene Wenger, Gerrard Houllier na Ruud Gullit hakika zimekuwa na mchango
mkubwa.
Ligi Kuu ya soka England (Premier League) mwanzoni ilikuwa
na klabu 22 lakini kukawepo na nia ya kutaka kupunguza idadi hadi 20 ili kuleta
ustawi zaidi na ubora katika ngazi ya klabu na kimataifa. Hii nia ikafanikiwa
mwishoni mwa msimu wa 1994/95 wakati vilabu vinne viliposhushwa daraja na na
viwili kupandishwa.
Timu ya Burnley ikapanda daraja mwaka 2009 na kufikisha
idadi ya timu ambazo zimewahi kushiriki Premier League kufikia 43. Timu yenye
mafanikio kuliko zote katika historia ya Premier League bila ya shaka ni
Manchester United. Ikiongozwa na Sir Alex Ferguson imeweza kunyakua mataji 11
na haijatokea ikamaliza ligi ikiwa katika nafasi chini ya tatu tangu kuanzishwa
kwa Premier League mwaka 1992


0 Maoni