NA,GOODLUCK CHRISTOPHER
Kufuatia mvua kubwa inayo endelea kunyesha mkoani
Katavi imepelekea kukatika kwa daraja la mto Makongoro linalo unganisha mitaa
ya kijiji cha Isubangala kata ya ilangu katika wilaya ya Tanganyika daraja
ambalo ni tegemezi kwa wananchi wa kijiji hicho na maeneo jirani.
Aidha nimebahatika kuzungumza na mkazi wa kijiji
hicho Living Atanaz ambae amesema kuwa
kukatika kwa daraja hilo ni adha kubwa kwa wakazi kwani wanashindwa kuvuka
upande wapili ili kupata huduma za msingi katika maeneo kama
Zahanati,Sokoni,Shuleni pamoja na Mashambani.
Kamera iliwanasa wanafunzi pamoja na watu wazima
wakiwa wameshindwa kuvuka richa ya wananchi hao kujaribu kutengeneza kivuko cha muda kwa kutumia miti jambo ambalo
bado lina leta hofu kwa wakazi hao.
Hata hivyo wananchi wameiomba serikali kuingilia
kati suala hili haraka iwezekanavyo ili kunusuru maisha ya wakazi wa kijiji
hicho pamoja na vijiji jilani ili shughuli ziweze kuendelea kama awali.
Nimegonga hodi katika ofisi za viongozi kijijini hapo ili kuzungumza nao juu ya suala hili bila mafanikio kwani tayari muda ulikua umekwisha na ofisi hizo zilikua zimekwisha kufungwa.





0 Maoni