Mwafrika Digital

https://youtu.be/ArXfq-5TVWA Subscribe Mwafrika TV

MTIBWA SUGAR YAICHAPA NDANDA FC 1-0

Mtibwa Sugar imefanikiwa kuibuka na ushindi kiduchu wa bao 1-0 dhidi ya Ndanda FC katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliopigwa Uwanja wa Manungu leo.

Kikosi hicho kimejipatia bao lake kupitia kwa Kelvin Sabato aliyefunga katika dakika ya 22 ya kipindi cha kwanza.

Wakata miwa hao wa Morogoro wamepata matokeo baada ya kupoteza mechi iliyopita dhidi ya Simba kwa kichapo cha bao 1-0.

Mtibwa sasa imefikisha jumla ya alama 33 kwenye msimamo wa ligi huku ikicheza michezo 23 na ikiwa nafasi ya 6.

Wakati huo Ndanda FC imekamata nafasi ya 12 ikijikusanyia alama 23 huku ikicheza jumla ya mechi 24 msimu huu.

Chapisha Maoni

0 Maoni