Waziri mkuu Mh. Majaliwa Kassim Majaliwa apiga marufuku usafirishwaji wa chakula hasa mahindi nje ya nchi.
Aidha waziri mkuu amewataka wakulima kutosafirisha mazao hayo kwakua wakifanya hivyo wanaweza wakasababisha janga la njaa kwa siku zijazo, maneno hayo aliyasema Moshi mkoani Kilimanjaro wakati wa sherehe za sikukuu ya IDD ELFITIR ambazo zilifanyika kitaifa mkoani humo.
Pia ametoa tahadhari kwa wamiliki wa magari yatakayo safirisha mazao hayo, kuwa magari yatachukuliwa na kupelekwa kwenye ghala la taifa na magari kupelekwa kwenye vituo vya polisi.
hivyo amesema kama kuna ulazima wakuuza basi wakulima waombe vibali kutoka wizara husika huku vibali hivyo vikitolewa kwa kuuza unga na si mahindi.
# Mc Goodluck

0 Maoni