Mwafrika Digital

https://youtu.be/ArXfq-5TVWA Subscribe Mwafrika TV

UCHAMBUZI

Kwanza niombe radhi kwa muonekano wa picha hii, huu ni uchambuzi mfupi kuhusu uhalifu unao endelea ndani ya mkoa wa Pwani.
       Kwanza nianze kwa kumshuru Mungu, serikali ya awamu ya tano chini ya raisi Dkt. John Joseph Pombe Magufuli kwa kuanza kuyatekeleza aliyo yaahadi wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, nishukuru jeshi la polisi chini ya IGP. Simon Siro kwa kuendea kuhakikisha ulinzi wa raia pamoja na mali zao unakuwepo wa kutosha.
         Kwa siku za  hivi karibuni nimekua nikikuta na hii picha ktk mitandao ya kijamii huku watu wakiiongelea kwa namna tofauti tofauti na maneno mengine yakiwa siyo mazuri kwa nchini yenye amani na utulivu kama hii  pengine maneno hayo yanaweza yakasababisha machafuko makubwa na watu pengine kuwa na visasi kwani mengine ni ya kichochezi huku mengine yakitolewa na baadhi ya waandishi wa habari wasio waadilifu hivyo mimi kama mwandishi wa habari ambae nimefumdishwa maadili nikaona si vyema kulifumbia macho kwasababu mauaji tunayoendelea kuyasikia yananiumiza na mimi kwakua wanao uliwa ni watanzania wenzangu hivyo haya ni maumivu kwa watanzania wote.
      Pengine unaweza usinielewe kwamba nini namaanisha, nikweli kwamba tumekua tukisikia watu kadhaa wakilipotiwa kuuwawa huku vifo hivyo vikihusishwa na itikadi za kisiasa.
      Kila mtu amekua akizungumza anavyo jisikia kuzungumza huku na baadhi ya wanasiasa  wakiwa wanasimama kwenye majukwaa na kuzungumza wanavyo fikiria juu ya mauaji haya lakini wakati mwingine tusipende kuzungumza kile tunacho jisikia kuongea bila kuwa na uhakika wa kile unacho kizungumza kwasababu naamini kwamba risasi moja inaweza ikaua watu wanao hesabika lakini neno moja la kichochezi linaweza likaua kizazi.
         Ni mda sasa wa watanzania wote, viongozi na vyombo vya ulinzi kukaa na kutafakari utatuzi wa mauaji haya lakini hatutofanikiwa kama hatujatafuta chanzo cha tatizo kwakua siamini kama tutatumia mabavu au maneno bila kujua chazo cha tatizo hii itakua ni kama kutwanga maji kwenye kinu.
         Sikuzote katika mambo kama haya huwa naamini kwamba hekima na busara nikitu cha msingi sana ili kujua chanzo na hatimae kujua ni jinsi gani ya kutatua mauaji haya pengine tusiliachie jishi la polisi pekee pengine wazee na viongozi wa dini nao wapewe nafasi waliangalie hili pamoja na wananchi kwa ujumla.
        N.B  Kumbuka kuwa katika mambo kama haya maimbi na sara ni jambo la mhimu sana pia busara inahitajika japo mabavu yanaweza kutatua swala hili ila inabidi tujue kwamba kwa mabavu huenda wakaumia sana na kwa wahalifu wote mnao fanya hivyo muogopeni Mungu na mkumbuke kuwa serikali ina mkono mrefu mnafanya uharifu leo lakini ipo siku mkono wa sheria utawafikia tu.
 
       
# Mc Goodluck

Chapisha Maoni

0 Maoni