Mwafrika Digital

https://youtu.be/ArXfq-5TVWA Subscribe Mwafrika TV

IMANI

Watu wengi tumekua tukimuacha Mungu mutoka na hali ya maisha ambayo tunaipitia tunasahau kuwa jaribu tunalo lipitia Mungu anajua kama tunaliweza.
      Mpendwa imani ni jambo zuri sana kwa kila binadam kwani pasipo imani huwezi fanikiwa kwa kwa lolote hata ukimwacha mungu sidhani kama itakua ni njia ya kupata furaha katika maisha yako zaidi ya laana tupu.
       Watu wengine tumekua tukijilaani kwa midomo yetu na kubaki tukimlaumu Mungu kumbuka kuwa katika kitabu cha mwanzo ukisoma vizuri unakuta kwamba ktk siku tano kila kitu kiliumbwa kwa neno isipo kua siku ya sita ambapo binadam alifinyangwa kutoka ktk udongo na kisha kumpulizia pumzi lakini hili siyo somo la leo, unaweza ukajiuliza kwanini nimeingiza maswala ya uumbaji lakimi mimi nataka nikueleweshe vizuri kwani binadam tumekua tukijisahau kuwa maneno yanaumba kwani nabii wakwanza katika maisha yako ni wewe mwenyewe hivyo yale unayo yakili ndiyo utakayo yapokea.
          Pengine nikuulize swali ni maneono gani malakwala umekua ukijitamukia ktk maisha yako?_____________.   Najua utanijibu mazuri,   lakini je, baada ya kuyatamka unayatimiza kwa vitendo na maombi? Hili litakua swali gumu kwako lakini.
           Jibu lake ni hivi kwa yale mema unayojitamkia juu yako yatatimia kama utayafanyia kazi kwa maombi, pengine utaniambia umesha ombewa na watumishi wengi lahasha mpendwa kama unajiwekea imani ya kuombewa tu aise utaombewa na wachungaji, wainjiristi, maasikofu, mitume na manabii n.k lakini utajikuta uko palepale cha mhimu lazima umwamini Mungu, kumwabudu kwa roho na kweli bila kusahau Maombi.
     Hebu jifunze kwa maneno ya huyo mtoto mdogo alieko pichani akiwa anamwambia mtoto mwenzie ambaye alikua amekata tamaa ya maisha na kumwacha Mungu.
      N.B kumbuka kuwa imani na maombi ni jambo ka mhim lakini endapo utamuacha mungu kwa kisingizio cha maisha mpendwa utaishia kupata laana na mafanikio kwako yatakua historia.

      # Mc Goodluck

Chapisha Maoni

0 Maoni