Ashukuriwe Mungu muumba mbingu na nchi kwa kunifikisha siku ya leo nikiwa hai na mwenye afya tele natumaini nawewe umzima waafya kama hauko vizuri kiafya nakumbea upate afya njema katika jina la Yesu ameni, nikukaribishe katika chapisho la leo kupitia kituo chako ukipendacho cha PLAN MEDIA, katika chapisho la leo nimegusia zaid katika swala zima la mafanikio ya kimwili na kiroho .
Tuanze kwa maombi. Baba katika jina la Yesu tazama ni wakati mwingine tena umenipa furusa na maono ya kuandaa somo hili naomba likawabadilishe watu sawasawa na mapenzi yako kwakua si kwaakili zangu au ujanja wangu bali ni kwa uweza wako, naomba baba umtume roho wako mtakatifu aniongoze niweze kuandika kitakacho mbadilisha msomaji kutoka hatua moja na kumpeleka hatua nyingine na uweze kumuongoza vyema atakae soma somo hili, naamini utafanya sawasawa na mapenzi yako baba nikushukuru katika jina la Yesu amen.
MAFANIKIO NINI?
Neno mafanikio lina maana nyini sana kulingana na uelewa wa mtu lakini kwa upande wangu nakupa maana moja wapo. Tunapokua tunazungumzia mafanikio ni hatua ya mtu kuyafikia malengo yake ambayo alikua anayatarajia au ni hali ya mtu kutoka katika hali duni kwenda katika hali iliyo nzuri kimaisha, kwamfano kutoka katika umaskini kwenda katika utajiri,kufauru masomo n.k.
Katika mafanikio kuna vitu vingi ambavyo mtu anapaswa kuvizingatia ili kuyafikia malengo yake hivyo naenda kukupa baadhi ya vitu mhimu vya kuzingatia.
>Kwa mtu yeyote ambae anapenda mafanikio nilazima ajitambue kwanza kwamba yeye ni nani akisha jitambua hapo itakua rahisi kufanikiwa kwani akiwa anajitambua atazingatia haya yafuatayo:
1:Muogope Mungu----Ijulikane kuwa Mungu yuko juu ya yote hivyo kama utakua humuogopi yeye na kumheshimu ndugu yangu mafanikio kwako yatabaki kuwa historia, hivyo inatakiwa katika kile unachoona kwamba kitaleta mafanikio kwako lazima umuogope yeye na kumshirikisha katika kila hatua unayo ipitia kwa maombi hapo mafanikio kwako utayaona.
Watu wengi wamekua wakitumia akilizao wakidhani kuwa wataweza na kusahau kuwa Mungu yuko juu ya yote na ndo sababu ya wengi wamekua hawafanikiwi kamwe katika maisha yao hivyo mpendwa muogope Mungu.
Mithali 9:10
2:Uwe makini kuchagua marafiki----Kusema ukweli marafiki nao ni sehemu kubwa ya mafanikio kwako kama ulikua hujui hili tambua hivyo lakini inategemea na ni marafiki wa aina gani ulio kuwa nao.
Watu wengi huwa wanadhani kuwa kila rafiki ni mwema kwake jambo ambalo huwa linawatesa wengi kwa kua wanajikuta wakichagua marafiki wabaya ambao huwarudisha nyuma katika mafanikio ndugu unae soma ujumbe huu hauwezi fanikiwa kamwe kama una marafiki wabaya zaidi watazidi kukurudisha nyuma kimaendeleo.
Si kila rafiki ni mwema kwako na sikila ane kuchekea ni mwema kwako wengine wana lengo la kukurudisha nyuma hivyo yakupasa kuwa makini na kuchunguza marafiki ulio nao.
Nakushauri kuchagua marafiki ambao ni wema kwa mafanikio yako hapo utajikuta ukifika pale unapo pataka ukizingatia hili utayaona mafaniko na Mungu akutangulie katika kuchagua marafiki wema.
Methali 13:20
3:Epuka kula na kunywa kupita kiasi(Anasa za dunia) ---- Hili ni jambo ambalo mala nyingi sana linawasababisha wengi kuto kufikia malengo yao kwasababu kama vitu hivi ukiviruhusu vikutawale mafanikio kwako yatakua historia.
Chamsingi unatakiwa uwe na kiasi katika mambo haya nakuhakikishia mafanikio utashindwa kuyahesabu ukizingatia haya utajionea mwenyewe.
Nakuombea kwa Mngu kama kuna pepo la anasa za dunia linakutawa basi litoke kwa jina la Yesu na nikushauri kuwaona watumishi walioko karibu nawewe nakuhakikishia utayaona mafanikio.
Methali 23:21
4:Fanya kazi kwa bidii----Kazi ni chanzo kikuu cha mafanikio katika maisha hivyo usitegemee mafanikio kama hufanyi kazi kwa bidi vijana wengi hawataki kufanya kazi na wengine wanachagua kazi wana sahau kua hata bitabu vya duni vinatwambia asie fanya kazi na sile hilo linajulikana kwa kila mtu.
Watu wengine hawafanyi kazi nashindwa kuelewa kwamba ni mafanikio gani yatakayo kujia mahali ulipo aise kama utakaa tu bila kazi mafanikio kwako itakua historia.
Ni wakati sasa wa kubadilika na kufanya kazi kwa bidii na sikukaa vijiweni ukizingatia hili mafanikio kwako utashindwa kuyahesabu na Mungu kutangulie.
2Watethelonike 3:10
5:Dhibiti ulimi wako--- Ulimi ni kiungo kidogo lakini huwa kinawaponza wengi kwa kushindwa kudhibiti kiungo hicho kidogo na kujikuta wakishindwa kuyafikia malengo waliyo yapanga.
Ulimi ni mzuri ukitumiwa vizuri lakini ukiutumiavibaya utaonekana mbaya hivyo watu wengine huwa wanapozwa na kiungo hicho kidogo.
Ushauri wangu kwako dhibiti ulimi wako ili uwe unazungumza au kutamka maneno ambayoyatakua ni mazuri na yenye tija katika mafaniko yako na wanao kuzunguka kumbuka kua ulimi unaumba pia utakacho kizungumza hakikisha kuwa kina baraka katika mafanikio yako.
1Petro 3:10
>Haya yalikua ni baadhi ya mambo ambayo mtu akiyazingatia na kuyafata kwa vitendo anaweza akayafikia malengo yake, nikushukuru kwa kusoma kunzia mwanzo mpaka hapa mwisho naamini kuna jambo umejifunza japo kuna wengine wata dharau na kupuuza lakini yote katika yote sifa na utukufu tumrudishie Mungu.
N.B: Kukata tamaa ni mwiko katika maisha tambua kuwa hakuna mafanikio yanayopatikana kirahisi hivyo changamoto utazipitia nyingi chamsingi usikate tamaa na kumshirikusha Mungu katika kila hatua kwa ibada,maombi na zaka.
#Mc Goodluck
Contact: +255 713 305 650
: goodlucmc999@gmail.com
planmedia@2017

0 Maoni