Mwafrika Digital

https://youtu.be/ArXfq-5TVWA Subscribe Mwafrika TV

UBOVU WA MIUNDOMBINU MKOANI MOROGORO

Wakazi wa manispaa ya mkoa wa morogoro kata ya lukobe mtaa wa mazimbu road walalamikia ubovu wa barabara ya mazimbu road campus .
               Wakizungumza na planmedia wamesema kuwa barabara hiyo kuna vifusi ambavyo vipo barabarani hapo kwa mda wa miezi mitatu jambo ambalo linawapa shida watumiaji wa vyombo vya moto na watumiaji kwa ujumla kupata shida ya kupishana kwa kutumia upande mmoja unaotumika kwa sasa.
              Mmoja wa watumiaji wa barabara hiyo ambae ni dereva wa pikipiki maarufu kama bodaboda, Athuman Mohamed amesema kuwa tangu kifusi hicho kimwagwe barabarani miezi mitatu iliyopita hakuna dalili yoyote ya kuikarabati barabara hiyo hivyo imekua nikero kubwa sana.
           Aidha amesema kuwa ubovu wa barabara hiyo unachangia kusababisha ajari na watu kuchelewa safari zao kwakua upande unaotumika ni mmoja tu badala ya pande mbili zinazo takiwa kutumika huku babara hiyo ikiwa na vumbi sana.
            Pia ameitaka serikali kuangalia ukarabati wa barabara hiyo kwani ina watumiaji wengi sana na kama watashindwa kuikarabati kwa sasa basi wawasaidie kureta greda ya kusambazia vifusi hivyo ili itumike pande zote mbili ili kupunguza kero hiyo.



          #Mc Goodluck

Chapisha Maoni

0 Maoni