NA.PATSON MWITA.
MCHEZAJI wa timu ya Bombom Fc ya Ilala, Suleiman Mohammed
anayefahamika kwa jina la Berko anayecheza
nafasi ya Golikipa namba moja wa timu hiyo,ambapo hadi sasa amedumu katika
klabu hiyo kwa muda wa miaka tisa[9],alianza kupenda soka tangu alipokuwa na
umri wa miaka kumi na miwili[12],kabla ya kuwa golikipa alikuwa anacheza nafasi
ya ushambuliaji lakini alivutiwa zaid na udakaji na golikipa wa yanga Yoberko
wakati huo akiwa mchezaji wa yanga.
Suleiman ambaye
amewahi kuwa mshindi wa tuzo ya mashindano ya JK yaliyofanyika mwaka jana na
kufanya kuibuka golikipa bora wa mashindano hayo,Bombom ilimfanya qweze
kushiriki mashindano mbalimbali kama vile COPA coca cola,JK inasifika kuibua
vipaji kama vile Ramadhani sigano kwa sasa anachezea Azam fc,Ibrahim ajibu
anachezea timu ya yanga na Hassan isiaka anayekipaga timu ya mtibwa sugar.
Akielezea mambo
asiyoweza kuyasahau Suleimani alisema’’sitosahau niliposhindwa kufuzu kucheza timu ya Taifa ya
vijana chini ya umri wa miaka kumi na saba 17[Serengeti boys];jambo lingine
ambalo sitoweza kusahau niliposhindwa kucheza soka kwa kipindi cha miezi
hisiyopungua miwili’’.hayo yamesemwa na Suleiman.
Timu aliyoifurahia katika maisha yake ya soka ni Bombom Fc anayoitumikia mpaka sasa,vile ilimpaumaharufuna
mafanikio alioyapata katika maisha yake ya soka;pia ametoa ushauli kwa
wachezaji chipukizi ambao wamekata tama kwenye soka na kuwaomba wasikate tama
na badala yake wafanye mazoezi ya kutosha
ili wafikie malengo yao kwenye soka.
[PICHANI NI GOLIKIPA WA BOMBOM FC SULEIMAN BERKO {KATIKATI}AKIWA NA WACHEZAJI WENZAKE.PICHA NA MAKTABA].



0 Maoni