
Wakazi wa yombo kilakala wilayani Temeke mkoani Dar es salaam wachoshwa na uchafunzi wa mazingira utokanao na viwanda katita mto yombo ambao husababisha uchafunzi wa mazingira pamoja na uchafunzi wa bahari ya hindi kwakua maji hayo hutiririka kuelekea baharini
.
Mmoja wa wakazi katika eneo hilo Bw. Seif Chekwa amezungumza na Plan Media na kusema kuwa mto huo umekua ukichafuka kutokana na maji machafu yanayo toka viwandani kutiririshwa na kuelekezwa katika mkondo wa mto huo jambo ambolo huchafua mto huo na mazingira kwa ujumla.
Aidha Chekwa amesama maji hayo hutoa harufu mbaya ambo nikero kwa wakazi wanao zunguka mto huo jambo ambalo ni hatari kwa afya ya wakazi hao pamoja na watoto wadogo wanacheza katika maji hayo machafu.
Mbali na hayo Chekwa amedai kuwa kutokana na uchafuzi huo unasababisha ongezo la mbu katika eneo hilo ambao huambukiza ugonjwa wa maralia kwa kiasi kikubwa ingawaje watu wanajitahidi kujifunika vyandarua nyakati za usiku wanapo lala.
Vilevile mto huo awali ulikua ukitumika katika shughuli mbalimbali zinazo wasaidia wakazi wa eneo hilo kama kuchota maji ya kutumia majumbani pamoja na shughuli za kilimo cha mbogamboga katika mashamba yaliyopo katika mbonde la mto huo hivyo shughuli hizo zimekatishwa kutokana na uchafuzi huo.
Pia Chekwa ameiomba serikali kuingilia kati suara hilo ili kukomesha tatizo hilo na kuhakikisha wamiliki wa viwanda wanatengeneza mfumo mzuri wa kuhifadhi maji hayo machafu ili kuunusuru mto huo pamoja na afya za wakazi hao
Kwa picha zaidi zinozo onosha hali harisi ya mto Yombo.






0 Maoni