
Wanafunzi wa chuo cha uandishi wa habari cha Time School of Journalism [TSJ] kilichopo Ilala mkoani Dar es salaam wanatarajia kufanya ziara ya kimasomo mkoani Tanga hapo tarehe 20/10/2017 ziara hiyo itafanyika tarehe hiyo apambopo ilisogezwa mbele kutoka tarehe 18/10/2017 kutokana na sababu ambazo zipo nje ya uwezo wa chuo hicho.
Pia kila mwanafunzi anatakiwa kilipia ziara hiyo kisi chapesa za kitanzania zisizo pungua 70,000 zitakazo fanikisha ziara hiyo ambapo wanafunzi wanaendelea kuchangia japo kuna wengine bado mpaka sasa hawajachangia pesa hiyo ingawaje serikari ya wanafunzi TSJOSO inaendelea kuwashawishi wanafunzi wote kushiriki ziara hiyo ambapo mwisho wa kuchangia pesa hiyo iotakua tarehe 16/10/2017 .
Aidha ziara hiyo italenga kujifunza kwa vitendo zaidi na kuonesha uwezo wao wawapo nje ya mazingira ya chuo kulingana na kile wealicho fundishwa darasani. Wanafunzi hao watatumia muda wa siku nne mkoani Tanga huku wakizungukia sehemu mbalimbali kama; Mapango ya amboni, Chemichemi ya maji moto, Hospitali ya Mombo, TK FM, Kiwanda cha maziwa cha Tanga Fresh pamoja na kiwanda cha theruji cha Tanga cement.
Vilevile waziri wa mambo ya nje katika chuo hicho Mh. Athony Mwasonge amesema kuwa zira itakua salama na wameshatafuta mazingira mazuri yakufikia nakulala katika siku zote ambazo wanafunzi hao wakiwa mkoani Tanga na uhakika wa kutembelea sehemu zote zilizotajwa hapo juu.
Wanafunzi wa stashada ya nne pamoja na astashahada yapili itakua ni ziara ya mhimu kwao kwasababu ni wanafunzi ambao wanaenda kazini pamoja na mazoezi kwa vitendo katika vyombo mbalimbali vya habari yaani [fielid] ambapo na mitahani yao ya mwisho maswali yatajikita zaidi katika ziara hiyo.
Wanafunzi wata pata nafasi ya kushiriki michezo mbalimbali, kuogelea baharini,kupiga picha,kula chakula kwa pamoja lakini pia watapata nafasi ya kuandaa vipindi mbalimbali vya runinga, redio pamoja na kuandika habari za kwenye gazeti .

0 Maoni