Mwafrika Digital

https://youtu.be/ArXfq-5TVWA Subscribe Mwafrika TV

TATIZO LA MAJI MOROGORO

NA. Gooodluck J Christopher


Wakazi wa Kihonda manispaa ya morogoro wame paza zauti zao wakilalamikia tatizo la maji ambalo limekua ni tatizo linalo watesa kwa  muda mrefu pasipo kutatuliwa ingawaje serikali inafahamu uwepo wa tatizo hilo na kushindwa kulifanyia kazi.
Mmoja wa wakazi hao ndugu Jonasi Eliasi Mkude amesema kuwa wanapata shida ya maji ambapo maji hutoka katika mabomba mala moja kwa wiki katika baadhi ya maeneo ambapo maeneo mengine maji hayatoki kabisa hasa maeneo ya kwa chambo, lukobe pamoja na mkundi.
Hatahivyo tatizo hilo la maji limesababisha kuibua ajira kwa vijana ambao wana chota maji kwa kutumia usafiri wa baisikeri,Guta pamoja na magari madogo kutoka maeneo ya Veta,Mbuyuni,Barabara mpya na Mazimbu ndani ambapo huuza maji hayo kwa kiasi shiringi 500 mpaka 1000 kwa dumu ama ndoo moja kubwa.


Vilevile ndugu Hadijah Ommary Nassoro  ambae pia ni mkazi wa kihonda amesema wamekua wkiletewa bili ya maji hata kama maji hayatoki jambo ambalo limekua kero sana kwasababu wanalipia maji ambayo hawayatumii kwasababu unakuta mtu analetewa bili ya maji kwenye bomba ambalo maji hayatoki kabisa.
Aidha kuwepo kwa tatizo hilo imesababisha wakazi hao kuchimba visima visivyo rasimi vinavyo toa maji ya chumvi ambo si safi na sarama kwa matumizi ya binadamu wanalazimika kutumia nmaji hayo ingawaje wanafahamu kuwa maji hayo si safi na salama kwa sababu baadhi yao hawana uwezo wa kumudu gharama za kununua maji kutoka kwa wauza maji kwa gharama iliyotajwa hapo juu.
Pia wakazi hao wameliomba shiraka la maji mkoani hapo MORWASA  kusikiliza kilio chao na kulitatua tatizo hilo halaka iwezekanavyo ili kunusuru afya za wakazi hao kwasababu maji ni uhai na pasipo maji hakuna uhai hivyo utatuzi wa tatizo hilo utaimalisha afya za wakazi hao  pamoja na shughuli mbalimbali zinazo tegemea maji.

Chapisha Maoni

0 Maoni