Na.Rashid Mongola.
Siku ya Alhamisi tarehe 12 kulikuwa na mchezo mkali katika uwanja wa Kinesi uliopo ubungo,mechi hiyo ilikuwa ya kirafiki kati ya timu ya Mshikamano ya daraja la kwanza ambayo inafundishwa na kocha Waziri Mahazi ilipambana na timu ya Makumbusho fc iliyopo ligi daraja la tatu ambayo ipo chini ya kocha John Mashaka.
Mchezo huo ulimalizika kwa jumla ya mabao 2 kwa 1 ambapo
makumbusho imeonjeshwa kichapo kutoka kwa wapinzai wao ambao wanashiriki ligi
daraja la kwanza.Mshikamano fc ilipata ushindi huo baada ya mchezaji Ali
Kabunda kupiga shuti kali dakika ya 32 na kufanya waongoze kipindi cha kwanza
kwa goli ,oja.
Kipindi cha pili kilianza kwa timu zote kushambuliana kwa
zamu huku Makumbusho wakionekana kuamka kwa kasi kwenye dakika ya 75 na
kuchomoa bao na kufanya mchezo kuwa mkali Zaidi,katika muendelezo wa
mashambulizi timu zote zikitafuta ushindi hatimae Wilson Wilege aliihakikishia
timu yake ya Mshikamano ushindi kwa kupiga bao zuri katika dakika ya 85 na
kufanya mchezo kumalizika 2-1.
Baada ya mchezo huo muandishi wetu alifanikiwa kuwahoji
makocha wa timu zote mbili,kwa upande wa kocha John alisema mchezo ulikuwa
mzuri ila kwa upande wake alisema alikuwa akijaribu kikosi,ila imekuwa tofauti
kwa kocha wa Msimamo fc Mahazi ambae akiwakilishwa na mshauri wa timu hiyo
alisema walikuwa wakijiandaa na mchezo ujao wa ligi daraja la pili dhidi ya
Mgmbo jkt ya jijini Tanga.

0 Maoni