
NI VIGUMU moja kwa moja kutoa nini maana kamili ya kujiamini?Kujiamini ni mtazamo wa mwanadamu dhidi ya binaadamu wenzake wanavyo mchukulia ,hii inaweza ikawa maana ya neno kujiamini.Ikiwa utajilinganisha na wengine hatimae ukaanza kuhisi aibu,basi ujue unakabiliwa na tatizo la aibu.
Kuna mambo mengi yanayoweza kumfanya mtu asijiamini mbele ya wenzake,kiasi cha kujishusha thamani na kujiona yupo
chini ya wenzake ,kwa jambo moja ama jingine na wakati mwingine humpelekea ashindwe hata kufanya mambo ambayo anayajua na kuyafanya kila siku,kisaikolojia huu ni ugonjwa ambao unaweza kuathiri uwezo wa mtu.
Nikiwa na maana kwamba mtu anaweza asiwe na ulemavu wa aina yeyote lakini akatembea upandeupande mbele za watu,pia anaweza akawa na akili lakini akashindwa kuzitumia kwasababu sio mtu wa kujiamini katika mambo mbalimbali anayoyafanya,kama ilivyo kwa magonjwa mengine yalivyo na tiba hata gonjwa hili la kutojiamini linatakiwa litibiwe.
Kujizoesha kujiamini ni moja ya tiba ya kujiamini,ambapo katika njia hii ya kumfanya ajiamini ni hali ambayo mtu anatakiwa asikilize maneno ya kutia moyo na yenye ujasiri ndani yake kutoka kwa watu maarufu kama vile;viongozi wa siasa,watetezi wa haki za binaadamu wanaotetea maslahi ya watu bila hofu.
Kukubali matokeo ni jambo ambalo linaweza kufanya mtu awe wa kuiamini,kwa maana pale unapokuwa na matatizo ambayo kila ukiyafikiria njia ya kuyatatua inakuwa ni vigumu na mwishowe hupelekea kuwa na mawazo ya kushindwa,hivyo unashauriwa pale utakapoona jambo fulani limekushindwa ni vyema kuliacha na kusonga mbele.
Kutembea kwa haraka ni njia mojawapo ambayo imethibitika inaweza kumuondolea mtu hali ya kutokujiamini,Haipendezi unapokuwa njiani mtu un atembea kama mgonjwa ama mtu aliyechoka,ukiwa hivyo ni rahisi sana kuwafanya watu wakukodolee macho ambayo yatakufanya ujihisi utofauti.Kutembea kwa haraka kuna faida nyingi ,lakini kubwa kabisa ni kuwafanya wengine wakuone wewe ni mtu wa kazi na usiyetaka kupoteza muda wako,kitaalamu mwendo unaoruhusiwa ni Wa asilimia 25,usizidishe sana kiasi cha kufanya uonekane unakimbia.

1 Maoni
Ha! Kumbe
JibuFuta