Wananchi wa jiji la Daressalaam wameiomba serikali kutilia
mkazo suala la usafi katika siku ya jumaamosi ambapo wananchi hao wameiomba
serikali ihakikishe watu wote wanafanya usafi katika mazingira badala ya
kujifungia ndani hadi mda wa saa nne unapofika ndio wanafanya shughuli zao
jambo ambalo limeonekana lipo kinyume na Agizo la mkuu wa mkoa Mh.Paul Makonda
linalowataka watu wote wa jiji hilo wafanye usafi
Wananchi wa jiji hilo wamekuwa na mitazamo tofauti kuhusiana
na usafi,ambapo baadhi yao wamesema
kuweka mazingira safi ni jukumu
la kila mwanachi, wapo waliosema kuwa mda uliowekwa sio rafiki hivyo ni bora
mda ukapunguzwa baada ya mwisho saa nne
iwe saa tatu kutokana na mda wa masaa mawili yaani saa kumi na mbili
hadi saa mbili ni muda unaotosha kufanya usafi.
Katika mahojiano na baadhi ya wananchi mwandishi wetu
alifanikiwa kuongea na mkazi wa Ilala jijini Daressalaam Ndugu Joseph .K. Christopher:”Alisema
kuwa ni kweli wanajua suala hili ni zuri kwa jamii kulifuatilia na kuhakikisha
kila mmoja anafanya usafi kwenye eneo aliopo ili kuepusha magojwa ya mlipuko
kama kipindupindu na Kuhara.
Akiongeza ndugu Joseph .K. Christopher amesema serikali
inalengo zuri na nchi yetu hasa jiji hili la Daressalaam amabalo watu wa nchi mbalimbali wanalitembelea,Pia uwepo wa Wizara
muhimu jambo ambalo linatakiwa kufanya jiji kuwa safi na kuendana na hadhi
yajiji lenyewe kuwa la kimataifa.hayo yalisemwa na mkazi huyo.
Pia mwandishi wetu alipata
kuongea na mmoja wa wafanya biashara Ndugu Said Sanze ambae ameipongeza
serikali pamoja na kusema kuwa ni sawa kabisa kutenga siku ya usafi na
ikiwezekana ziongezwe siku na kufanya sikuzote ziwe za usafi na kuweka wasimamizi
ambao watafuatilia kwa ukaribu hili
suala ili kuhakikisha kwa wale watakaoenda kinyue na sheria wanachukuliwa hatua
za kisheria.
Mwisho ni maoni ya wananchi wa Daressalaam ambapo kwenye
mahojiano na mwandishi wetu raia wameishauri
serikali iongeze nguvu kwenye suala hili kwa kutoa elimu kwa wananchi jinsi
gani hii siku ilivyo na umuhimu na pia waelezewe kuhusu faida ya kuweka
mazingira safi,Pia wamewaomba wananchi waishio jiji hilo kuachana na zana ya
kuwa wanaotakiwa kufanya usafi ni wafanya biashara pekee badala yake watoe
ushirikiano katika kuhakkisha jiji linakuwa safi.


0 Maoni