Daryo Prince
ni msanii wa bongo flava mzaliwa wa jiji
la Daresalaam ambae kwa sasa anatamba na wimbo
unaoitwa nyota yangu ambao ameurekodi katika studio ya US ambayo makazi yake yaliyopo Ubungo,ambapo amefanikiwa
kuufanyia video.
Wimbo wake
wa kwanza amerekodi katika studio ya US hatahivyo wimbo huo haukupata kufanya vizuri,akiendelea Daryo
ameiambia plan media sababu iliyopelekea
muziki wake kutopata nafasi ya kufika
mbali ni kukosekana kwa kupata nafasi ya kutosha kwenye vyombo vya habari.
Pia Daryo
amemuambia mwandishi wetu kuwa katika kufanya kwake kazi alifanikisha kufanya
wimbo unaoitwa acha niende kwa Diamond ambao
pia amefanikiwa kuufanyia video ambayo
inachezwa kwenye baadhi ya vyombo vya habari vilivyopo nchini na kupelekea
kupata mafanikio kama vile kuitwa kutumbuiza katika maonyesho mbalimbali.
Akielezea
mipango yake kwa sasa Daryo amesema anakazi inayokuja hivi karibuni ambayo
amefanikiwa kufanya na Goodkuck Gozbert
ambae ni msanii wa nyimbo za injili anetamba na kibao chake kinachoitwa
shukurani.
vilevile katika
ushauri alioutoa juu ya wasanii chipukizi
amewaasa waweke umakini katika kazi zao wanazozifanya ili kuhakikisha
wanaendana na kasi ya kibiashara iliyopo kwenye soko la muziki wa bongo flava
pamoja na miziki mingine,Pia ameiomba serikali iweke sheria za kulinda mali za
wasanii pamoja na kuwachukulia hatua kali wale wote wanao hujumu kazi za
wasanii.


0 Maoni