Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi( CCM) Mkoani Geita ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la
Geita,Joseph Musukuma na madiwani nane wa halmashauri mbili za wilaya ya Geita
wapo nje kwa dhamana baada ya kusota rumande kwa takribani siku sita.
Viongozi hao walipandishwa kizimbani leo Septemba
19, Mahakama ya Hakimu mkazi mkoani Geita,wakikabiliwa na makosa manne,Ikiwemo
kufanya mkusanyiko usio halali na kufunga barabara inayoelekea mgodi wa Geita
Gold Mine (GGM) hivyo kupelekea kiasi cha wafanyakazi wa machimbo hayo
kushindwa kufika kazini.
Washitakiwa wote
wamekana kutenda makosa hayo na kesi hiyo imeahirishwa mpaka itakapoitishwa
tena Oktoba 10, Mwaka huu.


0 Maoni