Mwafrika Digital

https://youtu.be/ArXfq-5TVWA Subscribe Mwafrika TV

MAKONDA KUBADILI JESHI LA POLISi KISASA, KATIKA KUKABILIANA NA UHALIFU




    [PICHANI MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM PAUL MAKONDA,ALIYEVAA SHATI JEUPE AKIWA SAMBAMBA NA JESHI LA POLISI.]PICHA NA MAKTABA.

KILIMANJARO.
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda leo amekabidhi gari 26 za polisi mkoani Kilimanjaro zilizopelekwa kwa ukarabati,ambapo gari hizo zimefanyiwa majaribio leo na zipo tayari safirishwa hadi Daresalaam kwa ajili ya matumizi ya kiusalama,mbali na kufanyiwa ukarabati gari hizo zimefungwa kamera maalumu zitakazo saidia jeshi la polisi kupata ushaidi Zaidi.

Wakati akiongea na moja ya chombo cha habari kilichopo hapa nchini,amesema anataka kuifanya Daresalaam kuwa jiji la kisasa na mfano kwa miji mingine,pia ameelezea juu ya mpango wa kufunga kamera katika vituo vyote vya mkoa huo ili kurahisisha shughuli za kiuchunguzi,  ambapo OCD , kanda maalumu, pamoja  na Mkuu wa Jeshi la Polisi  wataweza kuona kile ambacho kinafanyika.

Kazi kubwa ya gari hizo ni kupambana na uhalifu kwa kasi kubwa na kuweza kuwafikia wahalifu popote walipo pasipo na vikwazo,ambapo gari hizo zilizofungwa kamera  zitakuwa suruhisho kwa uhalifu jijini Dar es salaam na kupunguza ujambazi mkoani humo.

Chapisha Maoni

0 Maoni