Everton imemfungashia virago Ronald Koeman baada ya kupokea
kichapo cha mabao 5-2 siku ya jumapili kutoka
kwa washika bunduki wa London Arsenal,Taarifa kutoka kwenye uongozi wa
klabu hiyo inasema "ingependa kutoa shukrani kwa Ronald Koeman kwa huduma
aliyoitoa klabuni hapo kwa miezi 16 iliyopita".ambapo msimu wa ligi wa
mwaka 2017/2018 everton imeshinda michezo miwili pekee.
"Bado ninaamini ninaweza kubadilisha hali yote,"
Koeman alisema hayo kwenye mahojiano kabla ya mchezo wuliofanyika Jumapili,Koeman
anakuwa kocha wa tatu kutimuliwa kwenye klabu za uingereza msimu baada ya Frank
de Boer timu yake ilipofungwa na Crystal Palace na Craig Shakespeare timu yake
ilipofungwa na Leicester City.MDutchman
HUYO mwenye umri wa miaka 54, ambaye ameiongoza Everton hadi nafasi ya saba
katika msimu wa ligi uliopita licha ya kiasi cha pesa walichokitumia kufanyia
usajili ambapo Everton ilitumia kiasi
cha £ 140m wakati wa majira ya joto.
Mmiliki wa Everton Farhad Moshiri alimpa tumaini Koeman wiki
mbili zilizopita baada ya kushinda kwao 1-0
dhidi ya Burnley, lakini baada ya hapo walikutana na timu ya Brighton na
walipoteza pia ilipoteza na Lyon, katika
Europa League, kabla ya kuadhibiwa na Arsenal 5-2 kwenye uwanja wa Goodison
Parkl.
Siku ya Jumapili Koeman aliandika kuwa kupata matokeo dhidi
ya Arsenal ilikuwa "haiwezekani" baada ya mchezaji wao kutolewa
uwanjani na kufanya Everton kucheza pungufu wakiwa 10 uwanjani wakati huo likuwa
2-1.Huku nafasi ya Everton kufufuzu
kwenye Europa League ni ndogo, ambapo
ipo mwisho kwenye msimamo wa kundi hilo linalo zihusisha klabu za Merseysiders ,Atalanta,Lyon na Apollon
Limassol.
Mchezaji wa zamani wa Leicester City Steve Claridge, akizungumza
kwenye BBC Radio 5 aliiambia kuwa baada ya kupoteza kwa Everton siku ya Jumapili,"kunatakiwa
kufanyike mabadiliko ya haraka "Kwa
ushahidi huu, Everton ipo katika shida kubwa," alisemahuko Everton,pia
ameishauri timu hiyo ifanye usajili wa kutosha january mwakani ili kuiimarisha
klabu.


0 Maoni