UCHAGUZI WA MARUDIO WAAIHIRISHWA MAGHARIBI MWA
KENYA
Watu wawili wameuawa
kwa kupigwa risasi wakati wa makabiliano kati ya polisi na wafuasi wa upinzani
katika maeneo hayo.
Mwenyekiti wa IEBC
Wafula Chebukati amesema tume imechukua hatua hiyo baada ya upigaji kura
kutatizwa na ukosefu wa usalama.
Katika majimbo hayo ya
Kisumu, Siaya, Migori na Homa Bay, wafuasi wa upinzani walifunga barabara za
kuelekea katika vituo vya kupigia kura na kukabiliana na maafisa wa polisi siku
yote.
Katika baadhi ya
maeneo, makarani na maafisa wengine wa kupigia kura hawakufika vituoni kutokana
na kile mmoja wa wasimamizi alisema ni kuhofia usalama wao.
Serikali ilikuwa
imewatuma maafisa wa polisi katika maeneo mbalimbali kushika doria.
Gavana wa jimbo la
Kisumu Prof Anyang' Nyongo amewatuhumu polisi kwa kutumia "magenge ya
watu" kuwashambulia wafuasi wa upinzani.
Ameambia BBC kwamba
watu wawili wamefariki eneo lake na wengine 29 wanauguza majeraha.
Prof Nyong'o amesema
hawataruhusu uchaguzi wa marudio ufanyike katika kaunti hiyo.
"Nimetangaza kama
gavana wa hii kaunti wiki moja ya maombolezi ambapo wakati huo hakutakuwa na
sherehe. Kwetu uchaguzi huwa ni sherehe," amesema.
Amesema iwapo tume
hiyo itaendelea kusisitiza uchaguzi ufanyike, basi wataenda kortini kutaka
uzuiwe.
SOURCE. BBCSWAHILI.COM


0 Maoni