Gari la mwendo wa kasi
zaidi duniani laanza majaribio.
Gari lililoundiwa nchini
Uingereza linaloweza kukimbia kasi ya kilomita 1,610 kwa saa, linafanyiwa
majaribio yake ya kwanza huko Cornwall.
Bloodhound SSC linafanya mikimbio ya mwendo wa chini ya hadi
kilomita 320 kwa saa katika uwanja wa ndege wa Newquay.
Likiendeshwa na Andy Green, gari hilo linalenga kuvunja rekodi
ya dunia ya mwendo wa kasi zaidi ardhini.
Jaribio hilo litafanywa kwenye barabara maalum iliyojengwa eneo
la Nothern Cape nchini Afrika Kusini.
"Tumeunda gari lisilo la kawaida kabisa, lenye uwezo mkubwa
na kasi ya juu zaidi katika historia." Andy Green aliambia BBC.
Ni miaka 20 tangu mtu aendeshe gari lenye kasi kubwa duniani
katika jangwa la Nevada huko Marekani na kuandisha mwendo wa kilomita 1,227 kwa
sasa.
SSC
Gari hilo jipya limenufaika na teknolojia iliyoboreshwa kwa
miongo miwili na litasaidiwa na injini ya ndege ya vita ya Eurofighter-Typhoon
ambayo inatumia teknolojia ya roketi.
Bloodhound inataka kufanya jaribio la kuvunja rekodi ya sasa na
kuweka kasi kubwa ambayo hakuna mtu anaweza kuifikia au kuitazama
SOURCE. BBCSWAHILI.COM


0 Maoni