Mwafrika Digital

https://youtu.be/ArXfq-5TVWA Subscribe Mwafrika TV

MVUA YASABABISHA MAFURIKO DAR ES SALAAM

Na. Goodluck Christopher

Mvua  zinsazo fururza kunyesha katika jiji la Dar es salaam zimesababisha kuwakwamisha wakazi na watumiaji wa barabara ya morogoro road baada ya daraja la kibanda cha mkaa lilipo maeneo ya mbezi kufurika maji nakusababisha shughuli za usafirishaji kukwama kwa muda katika barabara hiyo.

Aidha mvua hizo ambazo zimefururiza kwa siku mbili zimeendelea kusababisha uharibifu wa miundombinu ya barabara na majumba katika eneo hilo la mbezi wakati huo mvua ikiendelea kunyesha jambo ambalo linaleta hofu kwa wakazi wa eneo hilo.

Vilevile wakazi wa eneo hilo akiwemo ndugu. Jonasi Razaro amesema kuwa mvua hizo ambazo zinaendele kunyesha zinaendele kufanya uharinifu mkubwa katika eneo lambezi hususa ni katika maeneo ya kibanda cha mkaa.

Pia Razaro ameongeza kwa kusema kuwa mvua kama zitaendelea kufururiza namna hii basi yatatokea maafa makubwa zaidi hivyo wale wanao ishi mabondeni katika eneo la kibanda cha mkaa na maeneo mengine ni heri wakachukua tahadhari mapema kabla maafa hayajawafika.

Hata hivyo mvua hizo zinazo endelea kunyesha katika jiji la Dar es salaam zinaendelea kusababisha mafuriko katika maeneo mbalimbali ya jiji hilo hali yakuwa ni kawaida kwa mafuriko kutokea marakwara pale tumvua  inapo nyesha.


Mamlaka ya hali ya hewa enaendelea kutoa tahadhari kwa wakazi waishio mabondeni kuchukua tahadhari kabla maafa hayajawakuta huku baadhi ya wakazi wakiwa wagumu wa kutii tahadhari hiyo inayo tolewa na marakwamara,









Chapisha Maoni

0 Maoni