NA.RASHID HASSAN
.
KOCHA wa timu ya Taifa ya Tanzania Salumu Mayanga ametaja
kikosi kitakacho ivaa timu ya Benin tarehe 11 mwezi wa 11 mwaka huu ambao
mchezo huo unatarajiwa kufanyika huko Benin huku Stars ikiwa ugenini katika
pambano hilo,mchezo huo utakuwa wa kirafiki baina ya nchi mbili ambapo kwa
Taifa stars inaingizo jipya la wachezaji akiwemo Yohana Nkomola na Ramadhani
Kabwili.
Kikosi hicho cha stars kinajumuhisha jumla ya wachezaji 24
ambao baadhi yao ni wachezaji vijana chipkizi wanaoinukia kwenye soka,kikosi
hicho kinaongozwa na;Goliki[pa,Aishi Manula,Peter Manyika na Ramadhani
Kabwili,Ulinzi unaongozwa na,Kelvin Yondani,Boniphas Maganga,Abdi Banda,Gadiel
Michael,Nurdin Chona,Erasto Nyoni na Dickson Job.
Viungo wanaongozwa na Himid Mao,Hamis Abdalah,Mzamiru
Yassin,Shiza Kichuya,Raphael Daud,Simon Msuva,IbrahimAjib,Mohamed Issa,Farid
Mussa na Abdul Mohamed,huku nafasi ya ushambuliaji ikikamatwa na Mbwana
Samatta,Mbaraka Yusuph,Elias Maguli na Yohana Mkomola.


0 Maoni