Burundi imekuwa taifa la kwanza mwanachama wa
mahakama ya kimataifa kuhusu uhalifu wa jinai kujiondoa katika mahakama hiyo.
Serikali ya taifa hilo la Afrika ya kati
liliuarifu Umoja wa Mataifa UN kuhusu hatua hiyo mwaka mmmoja uliopita , na hii
leo kujitoa kwao kunaanza kuidhinishwa rasmi.
Inaonekana kama kipimo cha jamii ya kimataifa
kuhusu haki.
Ni hatua sio ya kawaida.
Je kutakuwa na athari zake na ni kwa nini ni
muhimu?.
Kulingana na mwandishi wa BBC Anna Holligan
kujiondoa kwa Burundi ni majuto makubwa.
Mahakama ya ICC imeanza kutathmini iwapo
inaweza kuchunguza ghasia za kisiasa zilizoibuka baada ya rais Nkurunziza
kuchukuwa madaraka kwa awamu ya tatu, licha ya kuwepo kwa kipindi cha mihula
miwili katika katiba ya taifa hilo.
Image captionMakao makuu ya mahakama ya ICC mjini Hague
ICC bado ina uwezo kuchunguza uhalifu
uliotekelezwa wakati Burundi ilipokuwa mwanachama wa mahakama hiyo.
Lakini haiwezi kuchunguza uhalifu wowote wa
siku zijazo.
Hatua hiyo inaweza kuwa mfano na kuonyesha
viongozi wengine kwamba kujiondoa katika mahakama hiyo ni njia mojawapo ya
kuepuka jicho la kimataifa hadi pale Jamii ya kimataifa itakapochukua hatua na
taasisi kama vile Umoja wa Afrika ama baraza la usalama la umoja wa mataifa
litakapowafuatilia washukiwa na kuyakumbusha mataifa kwamba kujiondoa katika
ICC hakumaanishi moja kwa moja kwamba waathiriwa hawatopata haki.
SOURCE, BBCSWAHILI.COM


0 Maoni