Waziri mkuu wa
Uhispania Mariano Rajoy, amevunja bunge la Catalonia na kuitisha uchaguzi wa
mapema ili kurejesha hali kawaida katika eneo hilo.
Mapema Bunge la
Catalonia lilipiga kura kujitangazia uhuru kutoka Uhispania.
Hatua hiyo iliungwa
mkono kwa kura 70 -10 kura ambayo ilisusiwa na wabunge wa upinzani.
Waziri mkuu wa
Uhispania Mariano Rajoy, mapema aliwaambia maseneta kuwa udhibiti kamili
ulihitajika kurejesha sheria , demokrasia na udhabiti eneo la Catalonia.
Mzozo huu ulianza
wakati watu wa Catalonia waliunga mkono uhuru kwenye kura iliyokumbwa na utata
mapema mwezi huu.
Serikali ya Catalonia
ilisema kuwa asilimia 43 ya watu walioshiriki katika kura hiyo asilimia 90
waliunga mkono uhuru.
Lakini mahakama ya
katiba nchini Uhispnaia imeitaja kura hiyo iliyo kinyume na sheria.
Bunge la Uhispania
bado halijapiga kura kuamua ikiwa kwa mara ya kwanza litatekeleza kipengee cha
155 ya katiba ambacho kinairuhusu serikali kuchukua hatua zifaazo dhidi ya eneo
lolote ikihitajika.
Itairuhusu Uhispania
kuwafuta kazi viongozi wa Catalonia na kuchukua udhibiti kwa uchumi wa eneo
hilo, polisi na vyombo vya habari vya umma.


0 Maoni