Wakulima wawili wa
Afrika Kusini waliomlazimisha mtu mweusi kuingia katika jeneza akiwa hai
wamehukumiwa kifungo cha miaka 10 jela.
Theo Martins na Willem
Oosthuizen walihukumiwa mnamo mwezi Agosti kwa jaribio la mauaji na utekaji
nyara.
Walimtuhumu Victor
Mlotshwa kwa kupita katika ardhi, wakamshambulia na kumlazimisha kuingia katika
jeneza na kutishia kumchoma akiwa hai.
Kesi hiyo ilizua hisia
nchini Afrika Kusini na kuangazia wasiwasi wa ubaguzi wa rangi katika jamii
kadhaa za wakulima.
Bwana Mlotshwa
aliripoti kisa hicho baada ya kanda ya video kuhusu unyanyasaji huo kutokea
katika mtandao wa Youtube miezi kadhaa baadaye.
Katika hati ya kiapo
mahakamani wawili hao walisema kuwa hawakuwa na lengo la kumuumiza bwana
Mlotshwa wakati aliposhambuliwa mnamo mwezi Agosti 2016 na kwamba walitaka
kumpatia funzo.
Bwana Mlotshwa alikana
kupita katika ardhi yao, akisema kuwa alikuwa akichukua njia ya mkato kwenda
dukani ambapo alikuwa ametumwa na mamake.
Wakati wawili hao
walipohukumiwa , jaji aliiambia mahakama ilikuwa wazi kwamba walilenga kumuua
mwathiriwa.
SOURCE. BBCSWAHILI.COM


0 Maoni