
ZIMBABWE.
Zimbabwe
kutoa dola yake inayoitwa bond noti, lakini ilishuka thamani yake haraka
Wakati
dunia ikisubiri kuona ni nini kitatokea baada ya Robert Mugabe kukataa kujiuzulu
licha ya shinikizo kutoka kwa jeshi na chama tawala cha Zanu-PF party,
tunaangazia baadhi ya mambo muhimu unayopaswa kufahamu kuhusu nchi hiyo na hali
yake kwa sasa.
1. Uchumi umeporomoka.
Zimbabwe
imekuwa ikitoka katika mzozo mmoja wa kiuchumi na kuingia mwingine kwa kipindi
cha muongo uliopita. Viwango vya makadirio ya idadi ya watu wasio na ajira ni
tofauti, lakini chama kikuu cha wafanyakazi nchini humo kinadai kiwango cha
watu wasio na ajira kilikuwa asilimia 90% mapema mwaka huu.
Haki
miliki ya picha AFP/GETTY Image caption Zimbabwe...Watu wenye pesa zilizowekwa
kwenye benki kwa njia ya kieletroniki hawawezi kuzipata ama hupewa masharti ya
kikomo cha kiwango wnachopaswa kukito
Zimbabwe
imehangaika na hasara kubwa ya kiuchumi, iliyopanda mwaka 2008 ambapo kiwango
rasmi kilikuwa ni milioni sawa na asilimia 231 milioni . Nchi hiyo ililazimika
kuacha matumizi ya sarafu yake iliyoporomoka dhidi ya dola ya kimarekani na
hivyo kutumia sarafu ya kigeni.
Kutokana
na kuendelea kwa uhaba wa ukosefu wa fedha taslimu , serikali ilitoa dola yake
inayoitwa bond noti, lakini ilishuka thamani yake haraka.
Watu
wenye pesa zilizowekwa kwenye benki kwa njia ya kieletroniki hawawezi kuzipata
ama hupewa masharti ya kikomo cha kiwango wnachopaswa kukitoa. Kutokana na hili
biashara ya pesa kupitia mtandao wa intaneti imekuwa maaruifu.
2. Mugabe amekuwa mwenye utata kwa
muda.
Kiongozi
huyo mwenye umri wa miaka 93-aliwakanganya wakosoaji wake kwa kubakia
madarakani kwa muda mrefu sana. Wakati mwingine akipuuziliwa mbali kama kibonzo
anapokuwa ziarani katika nchi za ng'ambo, aliangaliwa na raia wa kawaida wa
Zimbabwe kama shujaa wa mapinduzi aiyepigana dhidi ya utawala wa wazungu walio
wachache na bado anapata heshma kama "baba wa taifa ".
Lakini
yeye na wafuasi wake wametumia ghasia kuendelea kumuweka madarakani, huku
wakitumia taasisi za serikali kumnadi bianfsi pamoja na chama chake.
Chama
chake kinasema kuwa kinapigana na ubepari na ukoloni, lakini matatizo ya
kiuchumi yamekuwa changamoto kwa taifa na wafuasi wake wameathirika pakubwa.
3.
Mke wake amesababisha kuangushwa kwa utawala wake
Haki
miliki ya picha Getty Images Image caption Mara kwa mara Mugabe alisema
ataondoka madarakani wakati ''ukombozi'' wake utakapo kamilika, lakini pia
anataka kumteua mrithi wake- jambo lililoibua mzozo wa sasa
Vita
vya kumtafuta mrithi wa Mugabe ambaye anaonekana dhaifu kutokana na umri wa
93wake viliimarika katika miezi ya hivi karibuni.
Chama
tawala kiligawanyika mara mbili , upande mmoja ukimuunga mkono mke wake Bi
Grace huku upande mwingine ukimuunga mkono mshirika wake wa muda mrefu,
Emmerson Mnangagwa.
4. Kiongozi mpya huenda asilete
mabadiliko yoyote.
Ikiwa
Bwana Mnangagwa aliyeng'olewa mamlakani atamrithi Mugabe kama rais mambo
hayatabadilika.
Alitajwa
katika maafa yote makubwa na mashambulio dhidi ya wafuasi wa upinzani
yaliyotekelezwa wakati wa azma ya kumuweka madarakani Bwana Mugabe.
Hata
hivyo , alidokeza kuwa anaweza kuanzisha mageuzi ya kiuchumi , na hata
kushirikiana na upinzani katika kuunda serikali ya mpito.
Haki
miliki ya picha Reuters Image caption Hatua ya kumfuta kazi Bwana Mnangagwa
ilionyesha dhahiri kwamba alitaka kumteua mkewe Bi Grace
5. Kilichotokea Zimbabwe yalikuwa
mapinduzi au la.?
Jeshi
liliingilia kati ghafla , hata hivyo bado hawajamuweka madarakani rais.
Katika
taarifa yake kwa Televisheni ,jeshi lilisema kuwa linachukua udhibiti wa nchi
kwa muda "kuwalenga wahalifu" wanaomzingira mkuu wa nchi, na si Bwana
Mugabe binafsi , na bado linamuita kama "amir jeshi mkuu".
Hata
hivyo hadi sasa, amekataa kuachia mamlaka, licha ya kwamba chama tawala cha
Zanu-PF kimemfuta kiongozi wake , na sasa bunge litalazimika kumshitaki
Hata
hivyo, Jumapili, Bwana Mugabe aliapa kubakia kama rais hadi pale mkutano mkuu
wa Zanu-PF, unaotarajiwa kufanyika mwezi Disemba utakapofanyika, kwa hivyo
haijawa wazi ni nini kitafuatia.
CHANZO BBC SWAHILI.

0 Maoni