
Na.Mandishi wetu.
Wanawake wameshauriwa kulala kwa kutumia upande katika miezi mitatu ya mwisho ya ujauzito wao ili kuzuia kujifungua watoto waliofariki tumboni.
Utafiti
wa zaidi ya wanawake 1000 ulibaini kuwa hatari ya mtoto kufariki tumboni
miongoni mwa wanawake wajawazito inaongezeka marudufu iwapo watalala kwa
kutumia mgongo wao miezi mitatu ya mwisho katika ujauzito.
Utafiti
huo ulichunguza mimba 291 zilizoharibika na wanawake 751 waliofanikiwa kupata
watoto.
Watafiti
wanasema kuwa upande ambao wajawazito hulalia ni muhimu sana na kwamba hawafai
kuwa na tashwishi yoyote wanapoamka na kugundua wamelalia migongo yao.
Takriban
mimba 225 nchini Uingereza huishia mtoto kuharibika na watafiti wa utafiti huo
wanakadiria kwamba takriban maisha ya watoto 130 kila mwaka yataokolewa iwapo
wanawake wataendea kulala kwa kutumia upande wa kulia ama kushoto.
Utafiti
huo wa MiNESS uliochapishwa katika jarida la Kujifungua ni mkubwa wa aina yake
na unathibitisha tafiti ndogo nchini New Zealnd na Australia.

0 Maoni