CHINA.
Shindano la malkia wa urembo
duniani la 2017 lilikamilika mjini Sanya China siku ya Jumamosi huku Mkenya
Magline Jeruto akishinda taji la malkia wa urembo barani Afrika.
Hatua hiyo inajiri baada ya
mwanadada huyo kutoka eneo la Elgeyo Marakwet nchini Kenya kuchukua nafasi ya
tano.
Taji la malkia wa urembo duniani
lilichukuliwa na mwanadada wa India Manushi Chhillar.
Andrea Meza wa Mexico alichukuwa
nafasi ya pili akifuatiwa na Muingereza Stephanie Hill huku naye Aurore
Kichenin wa Ufaransa akishinda nafasi ya nne.
Magline Jeruto ndiye mshindi mpya
wa taji la malkia wa Urembo barani AfrikaHaki miliki ya pichaFACEBOOK/JERUTO
Magline Jeruto ndiye mshindi mpya
wa taji la malkia wa Urembo barani Afrika
Magline Jeruto ambaye ndiye malkia
wa urembo wa Elgeyo Marakwet alichukua nafasi ya tano miongoni mwa wagombea 118
katika shindano la malkia mrembo dunia.
Mwanadada mwengine wa Afrika
ambaye aliorodheshwa katika nafasi kumi bora ni Ade van Heerden wa Afrika
Kusini ambaye alimaliza katika nafasi ya tisa



0 Maoni