KENYA.
Uamuzi wa mahakama ya juu wa kuidhinishwa kwa ushindi wa rais
Uhuru Kenyatta katika uchaguzi wa Oktoba 26 umezua maandamano ya ghasia katika
maeneo yanayodaiwa kuwa ngome za upinzani nchini Kenuya.
Kwa mujibu wa gazeti la Daily Nation wafuasi wa kiongozi wa
muungano wa Nasa Raila Odinga waliandamana ili kuonyesha kutoridhishwa kwao na
uamuzi huo.
Maandamano hayo yalibadilika na kuwa ya ghasia katika maeneo
kadhaa ya Nyanza, nyumbani kwa Odinga , katika maeneo ya Kibira na Mathare
mjini Nairobi.
Mjini Kisumu, gari moja la kibinafsi lilichomwa katika eneo la
Kondele muda mfupi baada ya ghasia kuzuka katika mji huo wa ziwa Victoria
kufuatia uamuzi huo wa mahakama.
kulingana na gazeti hilo vijana walifunga barabara zinazoelekea
mjini Kisumu kwa kuchoma magurudumu ya gari na mawe.
Waliwazuia watu watatu waliokuwa katika gari hilo la kibinafsi ,
wakawapiga na kuwaibia kabla ya kuliharibu gari hilo na kulichoma.
Watatu hao walikimbilia katika kituo cha polisi cha kondele
wakihofia maisha yao


0 Maoni