Takriban watu wanne wamethibitishwa kuuawa wakati wa
mashambulizi kwenye mtaa wa Mathare mjini Nairobi nchini Kenya
Wakaazi wa mtaa huo wa mabanda wanadai kuwa makundi yaliyokuwa
yamejihami kwa panga na silaha zingine yalivamia mtaa huo na kuwaua watu hao
ambapo pia waliharibu mali.
River Nairobi
Polisi wanasema kuwa wanachunguza kisa hicho na nia yake.
Wakaazi wanasema waliamka kwa mshangao asubuhi walipopata miili
ya watu wanne iliyokuwa na majeraha.
Kuuliwa kwa watu hao kumesababisha ghasia kusambaa hadi mitaa
iliyo karibu huku polisi wakikabiliana na wale waliokuwa wakilalamikia mauaji
hayo.
Kamanda wa polisi mjini Nairobi Japheth Koome alithibitisha
mauaji hayo na kusema kuwa uchunguzi unafanywa, lakini akatupilia mbali madai
kuwa yamesababishwa na ghasia za kikabila kufuatia hali ya kisiasa iliyopo
sasa.
Mauaji hayo yanatokea siku moja baada ya watu wengine watano
kuuwa wakati wa shughuli ya kumkaribisha kinara wa upinzani ambaye amekuwa
ziarani Ulaya na Marekani.
Polisi wanasema kuwa wale waliouawa walikuwa ni wezi waliopigwa
na watu waliokuwa na hasira.
SOURCE.BBCSWAHILI.COM


0 Maoni