Chama tawala nchini Zimbabwe Zanu-PF kimefuta Robert Mugabe kama
kiongozi wake. Kimemtua aliyekuwa makamu wa rais Emmerson Mnangagwa
ambaye alifutwa wiki mbili zilizopita kama kiongozi wake.
Kufutwa kwa Bw. Mnangawa kumezua mambo mengi huku jeshi likitwaa
madaraka na kumzuia Mugabe 93, kumteua mke wake Grace kama makam wa rais.
Maelfu ya watu nchini Zimbabwe waliingia barabarani siku ya
Ijumaa kuandamana kumpinga Bw. Mugabe.
Bw. Mugabe anatarajiwa kukutana na makanda wa jeshi na msafara
wa magari umeonekana ukiondoka makao ya rais.
Mkuu wa chama chenye nguvu cha wale waliopigania uhuru Chris
Mutsvangwa, aliiambia Reuters kuwa chama kilikuwa kinaanza mchakato wa
kumuondoa Mugabe madarakani kama rais.
Maelfu ya raia wa Zimbabwe jana walijitokeza barabarani hasa
mjini Harare katika jitihada za kuongeza shinikizo za kumtaka rais Mugabe
ajiuzuulu,wakishikilia mabango yaliyoandikwa Mugabe Must Go.
Zanu-PF ndio chama kilichomsaidia Mugabe kuwa madarakani nchini
kwa takriban miaka 40.
Lakini sasa inabidi wamshinikize ajiuzulu kufuatia mpasuko
mkubwa katika chama tawala.
Jeshi la nchi hiyo lilichukua hatamu za kiserikali na kumweka
Mugabe chini ya kizuizi cha nyumbani tangu juzi na wamekuwa wakifanya mazungumzo
ya kina.
Mugabe angependelea mkewe kumrithi lakini wapiganiaji wa uhuru
nchini humo wanamtaka aliyekuwa makamu wa Rais Emmerson Mnangagwa ambaye Mugabe
alimfuta kazi wiki iliyopita, kutokana na uhasama mkubwa baina yake na mkewe
rais Mugabe uliotokana na upiganiaji huo wa madaraka.
SOURCE.BBCSWAHILI.COM


0 Maoni