NA.RASHID HASSAN.
CHANGAMOTO
za maisha ni njia ya mafanikio kwa binaadamu hivyo ndivyo ilivyo na hakuna
anaepingana na huu ukweli ambao umedhihirishwa na kijana wa kitanzania Bwana
Omari Hafidhi ambae amepitia mengi katika safari yake ya maisha,ambae
anahistoria ya pekee baada ya kupanga vyumba takribani 15 kwa nyakati tofauti
lakini sasa ni moja ya vijana walio na
msaada mkubwa kwa vijana wengine.
Omari Hafidhi ni mzaliwa wa Pemba kaskazini,amezaliwa mwaka 1980
katika Hospitali ya wete,ambapo katika
upande wa mama yake yeye ni motto wa 6 na upande wa Baba ni mtoto wa 5,katika
familia yao alikuwa akilelewa na mama pekee,ambapo Omari alianza kujihusisha na
shughuli ndogndogo za kujipatia kipato
akiwa na umri wa miaka kumi na mbili[12]ili kuisaidia familia.
Alipofikisha umri wa miaka kumi na tano[15]alienda mjini
Unguja ambapo alikuwa akijihusisha na kazi ya uvuvi kwa mda wa miaka
isiyopungua sita,na baada ya hapo alienda jiji la Daresalaam mwaka 2000 ambapo
alikuwa akifanya biashara ya kuuza matunda akiwa kama mchuuzaji,alifanya
biashara hiyo kwa mda wa mwaka mmoja na hatimae alirejea tena Pemba.
Alipokuwa pemba alipatwa na tatizo la kupigwa na lisasi ya
mguu baada ya vuguvugu la maandamano ya kisiasa yaliyotokea 2001ambapo alisaidiwa na wasamalia wema na
kumpeleka hospitali ya Mnazi mmoja iliyopo Zanzibar na bnaadae alihamishiwa
Daresalaam kwa matibabu zaidi katika hospitali ya Muhimbili,baaada ya hali ya
kiafya kuimalika omari aliruhusiwa kutoka hospitali hapop.
Aliporuhusiwa alikuwa akiishi na mjomba wake Temeke ambapo
al;ikuwa akifanya biashara ya kuuza juisi katika mgahawa wa mjomba wake,na
baadae alihamia bugurni ambapo alipata kufungua mgahawa wake wa kuuzia juisi
baada ya kupewa pesa na kiongozi mmoja wa chama wa kisiasa alipokuwa anahitaji
nauli ya kiasi cha fedha tasiliumu za kitanzania shilingi 150,000 ili arudi
kwao lakini akaona kama fursa na baadae aliitumia pesa kuanzishia biashara yake
ya juisi.
Omari alifanikiwa kuiendeleza biashara yake ya juisi na
haimae alifanikiwa kuwaajili vijana wa kazi wasiopungua 26,ambapo aliongeza
vitu v1ya biashara na alikuwa akiuza vyakula mbalimbali pamoja na vinywaji
ambapo alikuwa amefungua Café iliyomuinua zaidi kimaisha na hatimae alifanikiwa
kununua gari mbili za abiria aina ya Costa,viwanja viwili chin na vingine
Pemba,pia amefanikiwa kujenga nyuma mbili ambapo zilizopo buguruni ambazo zina
thamani kubwa.
Pia omari amefanikiwa kumlea mtoto wa kaka yake aliefariki
2006,kwa sasa amefanikiwakumlea mtoto huyo ambaye kwa sasa yupo kidato cha
sita,pia omari ana watoto watano[5]ambao anaishi nao,pia hadi sasa amekuwa
akiendelea na biashara yake ya juisi ambayo imekuwa ni chachu kwenye mafanikio
yake,

0 Maoni