Mshambuliaji wa Manchester United Romelu Lukaku amekuwa mchezaji
wa Ubelgiji ambaye ameweka rekodi ya ufungaji mabao mengi kwa timu ya taifa
hilo.
Vijana hao wa Roberto Martinez waliifunga Japan bao 1-0 huko Brugge.
Lukaku , 24, alifunga goli la 31 kwa nchi yake pale alipomalizia
krosi safi kutoka kwa Nacer Chadli aliyoiingiza wavuni kwa kutumia kichwa.
Lukaku alikuwa ametoshana na Bernard Voorhoof na Paul van Himst
walipokuwa na magoli 30 kila mmoja wiki iliyopita.
Ubelgiji waliendeleza msururu wao wa kutoshindwa hadi mechi 15.
Mara yao ya mwisho kushindwa ilikuwa mikononi mwa Uhispania
mechi ya kirafiki Septemba 2016.
Kwengineko, Uholanzi walipata ushindi wao wa pili tangu kukosa
nafasi ya kushiriki katika Kombe la Dunia nchini Urusi walipopokeza Romania
kichapo cha magoli 3-0 huko Bucharest.
Mshambuliaji wa zamani wa Liverpool Ryan Babel alifunga bao lake
la kwanza la kimataifa tangu mwezi Mei 2008, pamoja na mchezaji mwenza Memphis
Depay na Luuk de Jong.
Mabingwa wa Euro 2016 Ureno walitoka sare 1-1 na Marekani,
wakicheza bila nyota wao Cristiano Ronaldo. Vitorino Antunes alikomboa bao
lililokuwa limefungwa na Mmarekani Weston McKennie mapema mwenye mechi Leiria
SOUCE. BBC SWAHILI.COM


0 Maoni