ZIMBABWE.
Spika wa bunge la Zimbabwe ametangaza
kuwa rais Robert Mugabe amejiuzulu .
Spika wa bunge Jacob Mudenda alisema
kuwa hatua hiyo ni ya kujitolea na amefanya hivyo ili kuweza kuwepo kwa
mabadiliko ya amani ya mamlaka kulingana na chombo cha habari cha Reuters.
Tangazo hilo la ghafla lilizuia
harakati za bunge kutaka kumng'oa madarakani ambazo zilikuwa zimeanza dhidi
yake.
Haki miliki ya picha AFP/getty Image
caption Nukuu ya rais Mugabe alipokuwa akijiuzulu
Kwa mujibu wa chombo cha habari cha
Reuters, Spika wa bunge amesema kuwa kiongozi mpya atawekwa madarakani siku ya
Jumatano.
Haki miliki ya picha AFP Image
caption Raia wa Zimbabwe wafurahia kujiuzulu kwa Mugabe
Wabunge walifurahia kufuatia hatua
hiyo na raia wameanza kusherehekea barabarani.
Je,ni Kiongozi mkombozi ,mfisadi au
mwonevu?
Awali bwana Mugabe alikuwa amekataa
kujiuzulu licha ya jeshi kuchukua mamlaka huku hatua hiyo ikifuatiwa na
maadamano ya raia waliotaka kiongozi huyo kung'atuka mamlakani wiki hii.
Amekuwa mamlakani tangu taifa hilo
lijipatie uhuru wake 1980.
Bwana Mugabe ameshinda uchaguzi wa
urais mara kadhaa lakini katika kipindi cha miaka 15 iliopita shughuli hiyo
imekumbwa na ghasia dhidi ya wapinzani wake.
Ameongoza kipindi cha uchumi
ulioanguka ambapo raia wamezidi kuwa masiki zaidi ya walivyokuwa 1980.
Haki miliki ya picha Reuters Image
caption Raia wa Zimbabwe katikati ya mji mkuu wa Harare wakifurahia kuzjiuzulu
kwa Mugabe
Hatua iliosababisha yeye kuanza
kung'atuliwa madarakani ni ile alipomfuta kazi makamu wake wa rais Emmerson
Mnangagwa wiki mbili zilizopita.
Hatua hiyo ilionekana na wengi kama
ya kutaka mkewe kumrithi.
Iliwaudhi viongozi wa jeshi ambao
waliingilia kati na kumweka rais Mugabe katika kizuizi cha nyumbani.
Ni Shangwe mjini Harare kufuatia
kujiuzulu kwa Mugabe
Waziri mkuu wa Uingereza Theresa May
amesema kuwa kujiuzulu kwa Mugabe kunaipatia
Zimbabwe fursa ya kuwa na mwanzo mpya kufuatia ukandamizaji uliotawala uongozi wa Mugabe.
Zimbabwe fursa ya kuwa na mwanzo mpya kufuatia ukandamizaji uliotawala uongozi wa Mugabe.
Amesema kuwa Uingereza ambaye ni
rafiki wa zamani wa Zimbabwe atafanya kila awezalo kusaidia kufanyika kwa
uchaguzi ulio huru na haki na kujenga uchumi wa Zimbabwe.
Haki miliki ya picha AFP Image
caption Rais Robert Mugabe ajiuzulu.
Ubalozi wa Marekani mjini Harare
umesema kuwa ni hatua ya kihistoria na kuwapongeza raia wa Zimbabwe kwa kutoa
sauti zao na kusema kwa njia ya amani kwamba ni wakati wa mabadiliko.
Chama cha upinzani nchini Afrika
Kusini cha Democratic Alliance kilifurahia hatua hiyo kikisema kuwa bwana
Mugabe alibadilika kutoka kuwa mkombozi hadi dikteta.
''Ninafuraha sana leo kwa sababu
nimekuwa nikiamini kwamba Mugabe atajiuzulu katika maisha yangu na
imefanyika'', alisema mwanaharakati wa haki za kibinaadamu Linda Masarira
aliyekuwa akizungumza na BBC.
.
.
''Na sasa kwenda mbele ni wakati wa
upinzani kujiandaa na kuona kwamba tunakuwa na serikali inayowajali raia
wake.Na kila mtu lazima ashirikishwe''

0 Maoni