NA.
GOODLUCK CHRISTOPHER
Muimbaji
wa nyimbo za injili Tanzani Baisa Mhela amelezea kuwa post yake katika akaunti yake ya
instagram kuwa siyo kiki na badala yake alikua anampa pole kipenzi cha moyo
wake Irene Uwoya kwa kumpoteza mme wake wahalali Ndikumana.
Siku
kadhaa zilizo pita mala baada ya Irene Uwoya kumpoteza mme wake wazamani
Ndikumana, Baisa aliandika maneno haya kupitia akaunti yake ya instagram “Kwa
kweli nakupa poleee sana @ireneuwoya8 Kwa kupotelewa na mme wako wa halali #ndikumana Kama bible inavyosema kwenye 1korinto
7:9+ yapaswa sasa uolewe kihalali na bible inaruhusu naomba uliweke moyoni
jambo hili nakusubili upate amani ya moyo tufunge ndoa iliyo halali achana nao
hao #ubongowaflavour Walikuharibu mpaka
kubadili dini njoo sasa tufunge ndoa
achana na huyo mhuni @dogojanjatz Njoo tudumishe pendo halisi nilikuota naona
nafasi yangu imefika sasa baada ya kupoteza ndikumana wako Njoo nisaidie kulea mwanangu #reneebaisa” mwisho wa kunukuu.
Baisa
hakuishia hapo alipost video inayo muonesha Irene uwoya akiwa analia huku
ukisikika wimbo wake Baisa Mhele unaofahamika kwa jina la #Usilie jambo ambalo liliibua hisia tofautitofauti
kwa wadau wa muziki wa ijili ndipo plan media iliamua kumtafuta Baisa
.
Aidha
amesema kuwa anampenda Irene Uwoya na ni vibaya kwa mkristo alie okoka kuelezea
hisia zake kwa mke wa mtu ila kwa wanandoa wowote wanaruhusiwa kuoa baada ya
mmoja wapo kufa na ndiyo maana ameamua kuweka hisia kwa uwoya baada ya kutimiza
kipengele hicho.
Vilevile
Baisa amesema yupo katika mazungumzo na Irene Uwoya mengine mashabiki wake
wataendelea kuyajua atakapo yaweka wazi baada ya uwoya kumruhusu kufanya hivyo
maana hawawezi kuropoka zaidi ya yate wasubirie mambo mazuri.
Pia
Baisa amesema kuwa watanzania waache dhana ya kusema kila jambo kuwa ni kiki
kwasababu siku hizi hata mtu anapo mpenda mtu imekuwa ni kiki na badala yake
watambue kila mtu anahaki ya kumpenda mtu wa hadhi yeyote.
Baisa
amemalizia kwa kusema kuwa ameokoka anampenda Yesu ni kijana ambae bado
hajaoa na anatarajia kuo mapema mwakani na mlengwa wake atatimiza agano
hilo kwa kadri atakavyo ongozwa na Roho
mtakatifu pia amewaomba mashabiki wake kumuombea mipango yake ikamilike mapema aweze kumleta ndani Irene
Uwoya.


0 Maoni