Mwafrika Digital

https://youtu.be/ArXfq-5TVWA Subscribe Mwafrika TV

NAMNA YA KUFUGA KUKU WA NYAMA

NA. GOODLUCK CHRISTOPHER

Katika ufugaji wa kuku mtuji wa kuanzia huwa ni tatizo kubwa sana hasa pale mtu anapo tembelea miradi mbalimbali ya watu wanao fuga kuku hao na wanapo jaribu kuuliza mtaji walio anza nao wanaogopa kwa kutajiwa mtaji mkubwa.

Siyo lazima wewe kuanzisha mradi Mkubwa kama unayo iona ya wengine. Hao mpaka kufikia hapo wamechukua muda kidogo na wamekutana na changamoto nyingi na hizo ndizo zime wafikisha sehemu hiyo unayo iona.

 Hivyo hata kwa mtaji mdogo kabisa unaweza kuazisha mradi wako wa ufugaji wa  kuku na baada ya muda nawewe utakuja kutembelewa katika mradi wako.
Katika ufugaji kuku kuna aina nyingi za kuku Leo tuangalie ufugaji wa kuku wa nyama [broiler].

Hivi ni vitu vya msingi na vya kuzingatia unapo hitaji kufuga kuku wa nyama [broiler] hivyo lazima uzingatie haya ili kufuga kuku ambao watakuletea faida kubwa pasipo kukuingizia hasara katika ufugaji wako.

Ø  Eneo, Upate eneo lenye hewa ya kutosha namwanga wa kutosha na joto la wastani ambalo ni rafiki kwa kuku hao kuishi
.

Mtaji, Lazima uwe na maji ya kutosha ambayo ni safi na salama kwa sababu kuku nao wanahitaji maji ya kutosha.


 Banda, Lazima uwe na banda ambalo ni safi na lenye ukubwa wa kuweza kuishi idadi ya hao kuku unao hitaji kufuga maana likibana sana watakufa wote.


Vifaa, Lazima uwe na vifaa vya kutosha vya kuwawekea chakula na maji na vya kufanyia usafi ndani ya banda la kuku hao
.

 Chakula, Hakikisha unawapatia chakula cha kutosha marakwamara ili wakue haraka na wenye na afya nzuri
.

Dawa, Hakikisha unawapatia chanjo marakwa mara ili kuwakinga na magonjwa mbalimbali yanayo weza kuhatarisha uhai kuku hao
.

Hayo ndio mahitaji kwa kuku wa nyama [broiler] hapa Leo hatuta ongelea hayo mahitaji, tutaongelea  gharama za matunzo kuanzia kununua vifaranga hadi kuuza na faida yake ipoje! Kwa kawaida watu hujua kufuga kuku ni mpaka uwe na mtaji Mkubwa lakini siyo hivyo, Hata mtaji wa Laki 5 unaweza fuga kuku [broiler]  na ukapata faida nzuri na jinsi utakavyo endelea kufuga mtaji wako utaendelea kukuwa zaidi.

Hapa tunaanza kwa mtaji mdogo wa kuanza na vifaranga 100
Kuna makapuni mengi yanauza Vifaranga. Kuna bei tofauti tofauti sh 1300 . sh 1400. Sh 1500.
Kwahapa tuna tumia Vifaranga wa bei ya sh 1400
Utanunua kifaranga kimoja 1400×100=140000


Siku umeenda kuchukua sasa unatakiwa huku nyuma uwe umekamilisha yafuatayo,
Banda umelisafisha vizuuri, na unatenga kona moja ambayo utaitengenezea umbo la nusu duara  (brooder) ndani ya brooder kutakuwa  maranda pia weka magazeti , magazeti husaidia maji ya kimwagika utaweza kusafisha kiurahisi bila kusahau vyombo vya chakula na maji  , chanzo cha joto unaweza tumia jiko la mkaa, balbu chungu au taa ya chemli.

 CHAKULA

Vifaranga 100 kwa wiki 4 au 5 unaweza tumia mifuko 5 ya kg 50 mpaka kuuzwa.

Wiki Mbili za mwanzo

Starter mash mfuko mmoja sh 60000 kwa mifuko miwili . 60000×2=
Sh 120000=

Wiki ya Tatu.

Growers pellet   mfuko mmoja  73,000/=.

Wiki ya 4
Finisher mash     57,000/= 57000×2=114000.

Jumla
 Sh 114000+73000+120000+140000=
Sh 447000

Dawa na kununua maranda ingharimu sh 53000.


Kwahiyo kwa matunzo hadi kuuzwa watagharimu sh 500000.

Katika kuuza kuku mmoja sh 6000 × 100=  Sh600000.
Faida ni sh 100000 kwa mwezi mmoja, utakavyo endelea kufuga  mtaji wako utaongezeka. Na utazidi kuwa mzoefu katika ufugaji wa kuku[broiler]. Pia bei ya chakula hutofautiana hii bei niliyoitumia ni hii baada ya chakula kupanda ila kuna sehemu chakula mfuko wa kg 50 inafika hadi sh 51000-54000..
Pia sio utasimamisha shughuli zako zote kwa ajili ya kuku.

Vitu vya kuzingatia kabla ya kuanza kufuga, chunguza kwanza soko lao lipoje kwahapo ulipo ili utakavyo wafuga kwenye kuuza wasije wakasumbua kuuza.


Chapisha Maoni

0 Maoni