Mwafrika Digital

https://youtu.be/ArXfq-5TVWA Subscribe Mwafrika TV

HAYA NDIO MAAJABU YA MAPANGO YA AMBONI

NA. GOODLUCK CHRISTOPHER

Ukiachana na Blazil Tanzania ni nchi yapili kwa kuongoza na vivutio vingi dunia na mapamgo ya ambani ni moja kati ya vivutia vinavyo patikana hapa nchini Tanzania, mapango hayo yanapatikana kasikazini mashariki mwa Tanzania katika mkoa wa Tanga
.
Vilevile mkoa wa Tanga ni moja kati ya mikoa iliyo barikiwa na vivutio vingi vya utali ikiwemo chemichemi ya maji moto lakini leo hii hatuto zungumzia  kivutio kingine bali tutazungumzia mapango ya amboni nikukaribishe sana katika makala hii fupi ambayo utapata kujione maajabu ya mapango hayo.

Mapango ya Amboni yaligunduliwa karne ya 16,taarifa  zilizopo ni kwamba watu wa makabila yaliyoishi jirani na eneo hilo, Wadigo,Wasambaa,Wabondei na Wasegeju,walikuwa wakiyatumia kwa ajili ya matambiko ya mizimu tangu Karne ya 16.

Eneo la Mapango hayo wakati huo lilijulikana kwa jina la Mzimu wa Mabavu,Watu kutoka sehemu mbalimbali ndani na nje ya Tanga, mpaka leo hii hufika mapangoni hapo kwa ajili ya  kutambika.

Kampuni  ya wazungu ya Amboni Limited,iliyokuwa ikimiliki mashamba ya Mkonge katika mkoa wa Tanga,ilimiliki eneo hilo la mapango mwaka 1892,ili kulitumia eneo hilo kama sehemu ya kupumzikia.

Serikali ya Tanganyika ilianza kutangaza eneo la mapango hayo kuwa eneo la hifadhi mwaka 1922,baada kujulishwa mapango hayo na wamiliki wa Amboni Limited.

Mwaka 1937 Serikali ilipitisha Sheria ya mambo ya kale (Monuments preservation ordinance of 1937) iliyofuatiwa na ile ya mwaka 1953 ambayo imesaidia kulinda mambo ya kale.

Mapango hayo yalitokana na  mabadiliko ya nguvu za asili ,zilizobadilisha maumbile ya miamba ya chokaa kipindi cha Jurasiki (Jurassic period) miaka milioni 150 iliyopita.

Kulingana na utafiti uliofanywa, eneo hilo la Mapango,lilikuwa chini ya maji miaka milioni 20 iliyota, na linakadiriwa kuwa na ukubwa wa kilomita za mraba zisizo pungua 234,lenye  mazingira ya uoto wa asili.

Utafiti uliofanywa Mturi (1975) njia ya kwanza ni ya maji ya Mvua yanapochanganyika na hewa ya [Carbondioxide] katika anga na kutengeneza tindikali ya kaboni (Carbonic acid) ambayo inauwezo wa kuyeyusha madini ya Calcium Carbonate yanayounda sehemu kubwa ya miamba ya chokaa.

Maji hayo yenye tindikali husababisha mabadiliko yanapoteremka kuelekea aridhini,yafikapo aridhini meza ya maji (Water Table) na yakiendelea kuongezeka,maji hayo yenye tindikali huwa na uwezo wa kuyeyusha maungio ya miamba,na sehemu laini zaidi za miamba na kusababisha nyufa.

Nyufa hizo huzidi kupanuliwa na maji yanayotembea na kusababisha baadhi ya  mawe kuporomoka na kufanya mapango, kasi ya maji inapozidi njia ndogondogo hupanuliwa na kuwa kubwa zaidi,na inawezekana mapango madogo madogo kuunganishwa na hatimaye kuwa na mfululizo wa mapango ya aina tofauti tofauti.

Zifuatazo ni baadhi ya picha zinazo onesha maajabu yaliyopo katika mazpango hayo na hapa tuaanza na mlango wa kuingilia ndani ya mapango hayo.
Hapa ni njee katika mlango wa kuingilia katika mapango haya na pichani ni mtalii wandani Goodluck Christopher.


Pichani hili ni eneo ambalo hutumika kwa ajiri ya matambiko, watu hutokea maeneo mbali mbali na kuja kufanyia matambiko kaika eneo hili.

 pichani ni eneo linalo fananishwa na mlima kilimanjaro, na unao waona pichani ni watali wa ndani kutoka chuo cha uandishi wa habari [TSJ] DSM.


 Pichani ni sehemu inayo fananishwa na myama jamii ya paka [CHUI] akiwa amelala.

MWAMBA unaokua na kuongezeka hasa katika kipindi cha Mvua,kutokana na mabadiliko ya kikemikali katika miamba ya Chokaa,inaongezeka kwa kiasi cha milimeta 7 katika kila miaka 100.

NJIA nyembamba iliyopo ndani ya Mapango,Conrad Fidelisi mtalii wandani akiwa anapita kwa tabu katika njia hiyo.



MWAMBA unaoonyesha Matiti YA mwanamke,ambao ni miongoni mwa vivutio vya watalii wa ndani na nje ya nchi.



BAO la kete ambalo lipo umbali wa futi 15 kwenda juu ya pango,ambapo watalii wengi huvutiwa na sehemu hii,ambapo Baba wa Taifa alikuwa shabiki mkubwa wa mchezo wa bao.


KOCHI (Sofa) la jiwe ambalo limo ndani ya Mapango ya Amboni, Goodluck na Sarafina wakiwa wamekaa katika Sofa hilo ambalo lipo katika kituo namba nne (4) kilichopo ndani ya mapango.


Huu ni mwamba uliojichonga ukawa kama msikiti na kuna maneno ya kiarabu kutoka kwenye kitabu kitakatifu cha Quroan.


Huu ni mwamba ambao umejichonga kama sanamu ya bikra maria pamoja na kitabu kitakatifu cha Biblia hivyo hufananishwa na kanisa.



Huu ni mwamba ambao umejichonga kama mnara wa marekani ambao ni maarufu sana kwenye maigizo ya kimarekani mara tu yanapo anza na jina la "CUROMBIA"


Huu ni mwamba wenye sura kama meli ambayo imetia nanga bandarini hatika sehemu ya chini.


Huu ni mwamba wenye sura ya ndege inayo beba abiria kukiwa kuna ngazi ya kupandia, mlango wa kuingia ndani kama inavyoonekana hapo pichani.




Hili ni jiwe lenye mfanano na makalio ya binadamu kama inavyoonekana pichani.




Huu ni mzizi wa mti ulio ingia ndani ya pango na kutengeneza alama ya mshale unao elekea kwenye mlango wa kutokea, kama mtu amepotea njia ndani ya pango anapo uona mzizi huo unaweza kumsaidia na kuikumbuka njia ya kutokea.


 
Hili ni pango la jinsia ambalo linaonesha picha zinazo fananishwa na jinsia ya kike na ya kiume za binadamu

Huu ni uoto wa asili unaopatikana nje ya mapango hayo.


Na huu ni mwisho wa makala yetu kwaleo ambapo tulikua tukizungumzia maajabu yaliyomo kitika mapango yaambani ambayo pia ni kivutio kikubwa cha utalii katika nchi yetu ya Tanzania ambapo watalii wa ndani na nje hutembelea mapango hayo na kuyashuhudia maajabu hayo yaliyomo, kumbuka kuwa hayo yalikua baadhi ya maajabu yayo patikana ndani ya mapango hayo panapo majaliwa tutakuletea maajabu mengine endelea kutufatia kupitia kituo chako pendwa cha plan media.


SHUKRANI ZA PEKEE ZIMUENDEE KILA ALIE WEZESHA MAKALA HII IKAMILIKE IKIWEMO KELVINI KIGADYE [MPIGAPICHA]  NA WENGINE WOTE WALIO SHIRIKI KWA NAMNA YEYOTEILE.



Chapisha Maoni

0 Maoni